![]() |
| Ofisa Habari na Mawasiliano Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Boniface Wambura. |
Na EmanuelMadafa
Taasisi moja kutoka Uingereza inayohusika
na kampeni dhidi ya upangaji matokeo kwenye mpira wa miguu (match fixing)
itafanya uwasilishaji (presentation) juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari
za michezo nchini.
Uwasilishaji
huo utafanyika kesho (Julai 5 mwaka huu) saa 11 jioni kwenye hoteli ya
Accomondia iliyopo Barabara Nkrumah jijini Dar es Salaam.
Wataalamu
hao wa kupiga vita upangaji matokeo ambao pia wataelezea jinsi matokeo
yanavyopangwa, jana (Julai 3 mwaka huu) walifanya uwasilishaji wao kwa wachezaji
na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys).
Taasisi hiyo yenye kibali kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) katika utoaji elimu ya kubaini
upangaji matokeo, vilevile inatoa elimu juu ya athari zinazopatikana kutokana
na upangaji matokeo.







Post a Comment