![]() |
Askofu Mkuu Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi
|
KANISA LA MORAVIAN TANZANIA,
JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI,
USHIRIKA WA BETHLEHEMU,
S.L.P. 905,
MBEYA
28/06/2014
ASKOFU ALINIKISA CHEYO,
JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI,
S.L.P 377,
MBEYA.
YAH: KUJIUZURU NAFASI YA UASKOFU ASKOFU
ALINIKISA CHEYO
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Baraza la Wazee Kanisa la Moravian Ushirika wa
Bethlehemu lililofanyika tarehe 28/06/2014 katika ajenda zake mojawapo
walijadili kuhusu mgogoro unaoendelea katika Jimbo la Kusini Magharibi. Wajumbe
walijadili kwa kina kuhusu mgogoro huo na kupitia mambo mengi hivyo waliamua
kuwa ili kulinusuru Kanisa kuendelea kuwa na migogoro isiyo ya lazima linatoa
tamko kuwa Askofu Alinikisa Cheyo ajiuzuru mora moja ili kuleta amani ndani ya
Jimbo letu.
Mchanganuo kuhusu mgogoro huo umeambatanishwa.
Tunakutakia utelekezaji mwema,
……………………………………………… …………………………………………
MWANDISHI M/KITI WA BARAZA LA WAZEE
USHIRIKA USHIRIKA WA BETHLEHEMU
Nakala
1. Mkuu wa Wilaya
2. Mkuu wa Wilaya wa polisi (OCD)
3. Wakuu wa Idara na Taasisi za Kanisa
4. Shirika zote za Jimbo
TAARIFA YA UCHAMBUZI WA MGOGORO WA HALMASHAURI
KUU YA JIMBO, JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI (JKM) DHIDI YA MWENYEKITI MCH. NOSIGWE
BUYA NA UHUSIKA WA ASKOFU ALINIKISA CHEYO
Ndugu zangu wapendwa, mgogoro huu umeleta madhara makubwa katika
Kanisa, na kuligawa Kanisa letu katika vipande vipande ambalo katika historia
yake. Mgogoro huu umesababisha kutoelewana kati ya uongozi wa Jimbo wao kwa
wao, Halmashauri kuu ya Jimbo, kamati tendaji na kuleta migongano kati ya
Kamati tendaji na Shirika, wachungaji kujigawa katika makundi. Hivyo mgogoro
huu umeleta uhasama kati ya mchungaji na mchungaji, ushirika na ushirika,
mchungaji na wakristo wake, uhasama usiokoma. Wachungaji kutoelewana na uongozi
wa Wilaya, Mtaa n.k. Hili jambo ni kubwa ingawa wengine wanatofautiana
kimtazamo, viongozi wa juu wa Kanisa, Wachungaji na Wakristo kwa ujumla. Lakini ukweli kuwa jambo hili ni kubwa
na lina madhara makubwa kwa Kanisa na endapo halitapatiwa ufumbuzi litazidi
kuleta madhara makubwa zaidi. Uchambuzi wetu kuhusu jambo hili tumeona kuwa
linamhusu sana Askofu Alinikisa Cheyo kuwa mhusika mkuu wa chanzo cha tatizo la
mgogoro huu kwa kukiuka Katiba ya Kanisa letu mara kadha, kiasi kwamba amebadilisha
nafasi yake ya Uaskofu na kuwa mtendaji mkuu badala ya kulisimamia Kanisa kwa ushauri na
usuluhishi. Yeye ameingia
kiutendaji zaidi na dhamiri ya kumuondoa Mwenyekiti Mch. N. Buya huku akijua
kabisa kuwa anafanya makosa ya kikatiba kwa kufanya mapinduzi, rejea Katiba ya KANISA LA MORAVIAN TANZANIA JIMBO LA
KUSINI MAGHARIBI IBARA YA 33, KUFUNGU B, Kipengele cha namba tatu ya kirumi (III) wajibu wa Askofu
“………….wote wanaweza kumwendea kwa shida zao za kiroho moja kwa moja, yeye
huwashauri, huwaonya, huwafariji na kuwaongoza kiroho bila kukata mambo yeyote
kisheria na kuyapeleka kwenye Halmashauri kuu ya Jimbo”
Pia alichukuwa nafasi ya
maamuzi ambayo yeye kikatiba siyo Mwenyekiti, hapa pia alikiuka Katiba, Ibara ya 33, Kifungu B, kipengele cha namba nane ya kirumi
(viii) “Rejea Katiba
“………….Anaweza kukaribishwa katika vikao vya kamati tendaji.”
Hivyo uchambuzi upo kama ifuatavyo:-
(a) Mwanzo wa chimbuko la mgogoro ilitokea mnamo tarehe 30/04/2013
ambapo Halmashauri kuu jimbo ilikutana Agenda ilikuwa kujadili utendaji mbovu
wa kamati tendaji. Na katika kikao hicho walimtaka Mwenyekiti atoe taarifa ya Tshs 200,000,000/= (millioni mia mbili) za Sekondari za ujenzi wa
shule. Na vilevile Makamu Mwenyekiti Z. Sichome alikuwa ameagizwa alete taarifa
ya maandishi ya jinsi anavyotimiza wajibu wake kikatiba, kusimamia majengo,
kufuatilia mkopo wa ujenzi wa Tshs Millioni mia mbili(200,000,000/=) , taarifa yake ikakataliwa maana haikuonyesha
jinsi alivyotimiza wajibu wake, rejea IBARA 35, KIFUNGU CHA 2wajibu wa Makamu Mwenyekiti kipengele F. “ Kuangalia kazi zote
za majengo katika Jimbo akishirikiana na Mwenyekiti wa Wilaya ambapo majengo
yapo na kutoa taarifa kwa Kamati tendaji kwa utekelezaji”. Kikao kiliona kina
uwezo wa kuamua maamuzi magumu bila kuvunja amani, hivyo Askofu aliamrisha
Kamati tendaji watoke nje ya kikao (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na katibu) kisha kikao kilikwenda
mbali zaidi kikamtoa mtunza hazina na mkaguzi wa ndani nje ya kikao. Hivyo safu
yote ya uongozi huo ikawa nje ya kikao. Baada ya hapo akachaguliwa Ndugu Hakimu
Mwandenuka kuwa Mwenyekiti wa kikao cha Halmashauri kuu ya Jimbo kwa uamuzi huo
ulikiuka Katiba Ibara 10: 2C rejea “Kamati tendaji” Mwenyekiti na Makamu wawe wachungaji” Imekuwaje Mkristo asiye Mchungaji achaguliwe
kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Jimbo? Na kwa nini Askofu A. Cheyo akubali
kukiuka katiba kiasi hicho?. Hapa inaonyesha kuwa Askofu ndiye chanzo cha
tatizo la mgogoro.
(b) Baada ya mazungumzo ya kikao, kamati tendaji na walotolewa nje
waliitwa kuingia kwenye kikao. Maamuzi yalikuwa:-
(i) Makamu Mwenyekiti Mch. Z. Sichome afuatilie
kwa makini kazi ya ujenzi na usimamizi wa majengo na atimize majukumu yake
kikatiba (Ibara ya 35:2F).
(ii) Mwenyekiti Mch. N. Buya asimamie vema majukumu
yake, na maamuzi ya Halmashauri kuu ya Jimbo ilimwagiza awapeleke Mahakamani
Ndugu Ambakisye Kabango na Dada Grace A. Mwalukuta kabla ya kikao cha tarehe
31/07/2013 vinginevyo maamuzi magumu yatachuliwa dhidi yake.
KUSIMAMISHWA MWENYEKITI N. BUYA
Kikao cha Halmashauri kuu ya
Jimbo kilikutana tena tarehe 30/07/2013 kikiongozwa na Mwenyekiti N. Buya.
Baadae katika mazungumzo Askofu Alinikisa Cheyo aliwaamuru Kamati tendaji
(Mwenyekiti, Makamu na Katibu), Mtunza hazina na Mkaguzi wa ndani watoke nje ya
kikao. Baada ya kutolewa wajumbe hao ndugu Charles Mwakipesile alichaguliwa
kuwa Mwenyekiti na Mch. Stephano Mbalwa kuwa mwandishi. Jambo la kushangaza kwa
makusudi kabisa Askofu alirudia kufanya jambo lile lile la ukiukaji wa Katiba. Uamuzi ukatolewa wa kumsimamisha Mch. N.
Buya kwa nafasi ya Mwenyekiti kwa sababu hajampeleka Ndugu A. Kabango na G.
Mwalukuta mahakamani kwa matumizi mabaya yaTshs 200,000,000/=, ambapo kikatiba mwenye kazi ya kutoa taarifa
za Vyuo na Shule za Sekondari Mbozi ni katibu alipaswa awajibike. Rejea Katiba Ibara ya 36, kipengele cha namba sita ya kirumi (vi)
kinasema “kupokea na kuzingalia taarifa za kazi za makatibu wa idara za umoja
wa wanawake ………….elimu ya kikristo, shule ya sekondari Mbozi na chuo cha
ufundi”
Rejea barua Kumb. Na KMT. JKM 2 ya tarehe 31/07/2013 yenye
kichwa cha habari kisemacho YAH: KUSIMAMISHA MCH. N. BUYA UONGOZI iliyowekwa
saini na Ndg. Charles Mwakipesile ambayo haikuwa na muhuri wa Ofisi ya Jimbo,
ikimtaka Mwenyekiti akabidhi Ofisi kwa Makamu Mwenyekiti. Hapa tunahoji Ndg. C. Mwakipesile alimwandikia Mwenyekiti N. Buya barua
akiwa kama nani na kwa Katiba gani?
Kwa ujumla unaweza kuona Askofu A. Cheyo jinsi alivyoendelea
kulitumbukiza Kanisa kwenye mgogoro mkubwa inakuwaje maamuzi ya kumsimasisha
M/Kiti wa Jimbo aliyechaguliwa na Sinodi asimamishwe na kuandikiwa barua na
mjumbe wa wakristo? Je Askofu analiona hilo kuwa ni jambo dogo? Askofu A. Cheyo
anajihesabu anatoa ushauri, anatoa ushauri gani kwa Kanisa kuona mambo yanaenda
hivyo kama katiba inavyomtaka katika Ibara ya 33 kifungu cha wajibu wa Askofu, kipengele cha iii, “……yeye hushauri, huwaonya,
huwafariji na kuwaongoza kiroho bila kukata mambo yoyote kisheria wala
kuyapeleka kwenye Halmashauri kuu ya Jimbo” Tuonavyo sisi Askofu Cheyo amepania
kuligawa Kanisa, ametoka kabisa kwenye wajibu wake, Ibara ya 33 …Askofu ni “ mhudumu wa Kanisa la umoja wa ndugu (Unitas
Fratrum) akikaa katika Jimbo lake na kuongozwa na Katiba ya Jimbo chini ya
Kanisa la umoja wa ndugu” kama ni hivyo mbona sasa haongozwi na Katiba na
anakiuka Katiba ambayo yupo chini yake
TAARIFA YA TUME ILIYOUNDWA NA HALMASHAURI KUU YA JIMBO KUCHUNGUZA TUHUMA ZA
MWENYEKITI MCH. N. BUYA.
Mnamo tarehe 20/11/2013 Halmashauri kuu katika kikao chake ilipokea taarifa ya Tume,
iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume Ndugu Hakimu Mwandenuka. Taarifa ya Tume ilibeba
mambo makuu mawili kama
ilivyokuwa imeelekezwa na Halmashauri kuu ya Jimbo kuyachunguza juu
Mwenyekiti Mch. N. Buya ilikuwa
kama ifuatavyo:-
a) Tuhuma kuwa Mchungaji Noswigwe Buya kushindwa
kusimamia masuala ya fedha.
b) Kutosimamia maamuzi ya Halmashauri kuu ya
Jimbo
Tume baada ya uchunguzi ilibaini kuwa Mwenyekiti Mch. N. Buya hahusiki katika ubadhilifu
wowote na wala hakuna ushahidi wowote
ulioonyeshwa yeye kuhusika, isipokuwa Tume iliwatuhumu Makamu M/Kiti na Katibu Mkuu kuwa
hawakuweza kusimamia na kumsaidia Mwenyekiti alipokuwa hayupo. Hivyo kulikuwepo uzembe wakati wa uongozi wake. Rejea Taarifa ya Tume Ukurasa wa 23
(nukuu),
1.
Tume ibaini kuwa
katika tuhuma mbili zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti Mch. N Buya zilizohusiana na
mkopo wa Tshs. 200,000,000/- na kushindwa kusimamia suala zima la fedha,
imebaini kuwa Mwenyekiti hakuhusika wala hakuna ushahidi wowote wa kufuja fedha
hizo bali imebaini kuwa kulikuwa na uzembe katika uongozi wake kusimamia hayo.
2.
Tume imebaini kuwa
Makamu Mwenyekiti Mch. Z. Sichone na Katibu Mkuu Mch. W. Mwansile hawakutimiza
wajibu kikatiba wa kumsaidia Mwenyekiti katika masuala hayo hasa pale
Mwenyekiti alipokuwa hayupo.
Taarifa hiyo Askofu aliikataa na kuelekeza shutuma zake moja kwa moja kwa Tume kuwa Tume
imembeba Mch. N. Buya, jambo hilo lilizua mgawanyiko katika Halmashauri kuu ya Jimbo. Wajumbe
wakataka kura ipigwe ya kumrudisha au kumwondoa katika wadhifa wake, Askofu
alikataa akasema; kura haitatupa majibu sahihi. Hivyo kura
haikupigwa. Kikao hicho kiliahirishwa mpaka tarehe 20/12/2013. Wakati wajumbe kikao hicho Askofu alianza kukutana na wajumbe wachache
wachache wa Halmashauri kuu ya Jimbo ili
kuwashawishi wasimrudishe Mch. N. Buya. Kikao kilifanyika tarehe
30/12/2013.
Katika uchunguzi wetu tumeona jinsi Askofu alivyo kwenye mstari
wa mbele kuigawa Halmashauri kuu ya Jimbo na kuendelea
kushirikilia msimamo wake wa kutomtaka Mch. N. Buya kurudi kwenye wadhifa
wake. Na ametumia njia ya kuwagawa Halmashauri ili kwake iwe rahisi kuitawala
na ni kinyume cha Katiba. Askofu hatakiwi
kuingilia utawala na kuwa mtawala bali awe
mpatanishi, tunajiuliza katika hili je amefanya upatanishi gani?
KUONDOLEWA UONGOZI M/KITI MCH. NOSIGWE BUYA
Mnamo tarehe 30/12/2013 kikao cha Halmashauri kuu ya
Jimbo kilikutana, katika kikao kile kilifikia hatua ya kumwondoa Mch. N. Buya
kwenye uongozi wa kuwa Mwenyekiti,
kinyume na Katiba. Katika
Katiba hakuna kifungu
kinachoruhusu Halmashauri kuu
kumwondolea dhamana ya Mwenyekiti uongozi
bali kama Board itaona anatuhuma za kimaadili
au vitendo vinavyoonyesha kujitenga kwake. Katiba inatoa maelekezo kuitishwa kwa Sinodi ya pekee
kwa uamuzi rejea Katiba ya Ibara ya 9, kifungu cha 3 kipengele cha (iii) “Sinodi ya pekee yaweza kuitishwa wakati
wowote na Halmashauri kuu ya Jimbo (PB) kwa kutoa taarifa ya miezi isiyopungua miwili. Sinodi hii
itashauriana tu katika jambo ambalo kwalo imeitwa “ lakini katika kikao kile
askofu A. Cheyo aliamuru kura ipigwe ili kumwondoa Mwenyekiti, tunajiuliza je
Askofu kufanya haya haoni
alikiuka Katiba?. Ikumbukwe kuwa kikao cha tarehe 20/11/2013 wajumbe walipendekeza kura
ipigwe, lakini Askofu alikataa, baada ya
kuona wajumbe wengi wameikubali
taarifa ya Tume lakini baada ya ushawishi wake kwa baadhi ya wajumbe, kikao cha tarehe 30/12/2013 akawashawishi wajumbe wapige kura.
Ukiangalia muda tulipofanya Sinodi ya uchaguzi ya Mwaka 2012 na mwezi wa nne 2013 si muda
mrefu kwa hiyo tathimini ya
kazi yake kwa Mch. N. Buya alianza tangu nyuma. Kama ni hivyo kwanini asitoe
hoja yake mbele ya Sinodi kuwa hana imani na Mch. N. Buya mpaka akasubiri
achaguliwe na ndipo aanze mizengwe?. Hapa inaonyesha wazi jinsi Askofu
anaonekana wazi jinsi anavyotumia vibaya wadhifa wake wa Uaskofu kulivuruga
Kanisa.
Jambo la kushangaza katika barua iliyoandikwa na Mch. Zakaria Sichone Makamu mwenyekiti ya
kuondolewa wadhifa wa kuwa Mwenyekiti Mch. N. Buya. Mch. Sichone anataja kuwa Mch. N. Buya
ameondolewa kwa makosa 11 (kumi na moja) bila ya kuyataja kurejea yale mawili yaliyochunguzwa na Tume, je haya makosa 11 (kumi na moja)
yametoka kwenye Tume ipi? na iliyoundwa na nani? Badala ya ile ya kwanza
iliyoongozwa na Ndg. Hakimu Mwandenuka? Je, Askofu ameziona njama hizo au
hazioni na kama ameziona ameyashughulikia kwa kiwango gani? Tunadiriki kusema
yeye anajua na amekubali uchafu huo ufanyike ili kulichafua Kanisa
JITIHADA ZA KUTAFUTA SULUHU LA KUTATUA MGOGORO
a) Tarehe 18/01/2014 Mch. N. Buya Mwenyekiti
aliitisha Sinodi katika Ushirika wa Bethlehemu (barua ya tarehe 2/01/2014)
aliomba iitishwe Sinodi ili kutoa maelezo kwa
maamuzi ya Halmashauri ya kumsimamisha.
- Lengo lilikuwa Sinodi iliangalie jambo hili
ili suluhisho lipatikane, kama
Katiba inavyosema. Ushirika wa Bethlehemu ulipokea ombi
hilo na kuwa tayari kuchangia
chakula. Kwa kipindi hicho
jitihada mbalimbali ziliendelea na watu mbalimbali kuishauri Kamati tendaji na
Halmashauri kuu kuliangalia jambo hilo lisilete mgawanyiko. Hivyo Sinodi ilitangazwa kwa njia ya Barua, Redio Baraka FM na Mch. N. Buya.
Askofu Alinikisa Cheyo aliingilia kati baada ya
kupata taarifa kuwa Sinodi imeitishwa, alimwagiza Mch. Z. Sichone akasitishe
tangazo Redio Baraka FM lisiendelee
kutangazwa na aliporudi kutoka ziara yake Iringa, alikwenda yeye na Makamu na Katibu walipinga na
kutangaza kuwa Sinodi siyo halali, Askofu akiwa mstali wa mbele kiutendaji. Katika hili linatupa picha halisi inaonyesha jinsi alivyohama
kwenye huduma ya Uaskofu na kujiingiza kwenye kamati ya utendaji kwa kufanya
hivyo amekuwa kinara wa mgogoro.
b) Usuluhishi wa Mch. Angolwisye Malambugi (M/Kiti Mstaafu) juu ya jambo
hili liliendelea kuvuta
kasi ya mgogoro akiingilia kati na kuwakutanisha kamati tendaji na Mch. Nosigwe
Buya ili walitengeneze jambo hilo, katika mazungumzo hayo walifikia muafaka kuwa M/Kiti Mch. N. Buya arudi kwenye nafasi
yake na Jambo hilo liende
Halmashauri kuu ya Jimbo kupata baraka ya ridhaa yao. Na
kumsisitiza Mch. N. Buya aandike barua ya kusitisha Sinodi iliyoitishwa na wakapatana kwenda Baraka FM kutoa sitisho hilo kwa lengo la patano hilo. Pamoja na jitihada zote hizo kikao cha Halmashauri kilipokutana na Askofu A. Cheyo aliporudi toka Kenya. maamuzi katika Halmashauri hiyo yalikuwa ya peke yao hawakuwa tayari
kukutana na Malambugi msululishi wa mgogoro huo bali uamuzi wao ulikuwa kinyume
na patano na kuamua:-
(i) Mch. N. Buya asirudishwe kwenye nafasi yake
(ii) Mch. N. Buya apangiwe kituo kingine cha kazi
aende Elimu ya kikristo akufundishe shuleni
(iii) Ahame kwenye nyumba anayoishi aende sabasaba
nyumba anapokaa Chimwemwe Mkurugenzi wa Radio Baraka F.M/
Tarehe 29/01/2014 Makamu mwenyekiti Mch. Z. Sichome alimwandikia barua Mch. N. Buya ya kumtaka ifikapo
tarehe 07/02/2014 awe amehama kwenye nyumba anaiyoishi.
c) Katika kutaka kutatua mgogoro huo, kundi la
wachungaji lilijitokeza kwa kujaribu njia mbalimbali wengine kwa kuandika barua
kupeleka Jimboni, wengine kwa meseji za simu n.k. pamoja na yote hayo
wachungaji wapatao 25 waliandika pingamizi lao kuhusu maamuzi yaliyochukuliwa
na Halmashauri kuu :-
(i) Kusimamishwa Uenyekiti wa Jimbo Mch. N. Buya
(ii) Kupangiwa kituo kipya cha kazi maana Sinodi
ilikwisha mpangia kituo hivyo hawezi kuondolewa bila ridhaa ya Sinodi
(iii) Kupinga uhamisho aliopangiwa Mch. N. Buya.
d) Wakristo na Mabaraza ya wazee nao
walijitokeza kwa nyakati tofauti kujaribu kuwaona Kamati tendaji kuomba
waitishe Sinodi ili kutatua mgogoro huo. Yote haya yaligonga ukuta, Askofu A.
Cheyo alikataa kuitisha Sinodi na kuona kuwa hakuna tatizo lolote na kusema
Wachungaji hao hawajui Katiba. Hayo aliyasema
kwa nyakati tofauti akiwa Kenya kwa njia ya mtandao wa Redio bomba FM na katika
vikao alisema hawezi kuitisha Sinodi pia Shirikani aliendeleza sentesi hizo.
Tunajiuliza hivi kweli
huyu Askofu analitakia mema Kanisa hili? Anakataa njia za mazungumzo,
anakatakaa upatanishi, anatakataa Sinodi ambayo ndicho chombo cha mwisho cha
kutatua matatizo ya Kanisa, Je Askofu amepotea kiasi gani? Haya yote anafanya
kwa makusudi, kwa nini anahofu Sinodi?
USULUHISHI WA MH: MKUU WA WILAYA NA MKUU WA POLIISI (OCD) Mkuu wa Wilaya (W) ya Mbeya Mheshimiwa
Dr. Normam Sigalla
aliitisha kikao na wajumbe wa Kamati tendaji, Askofu Cheyo, Mch. N.Buya na
uwakilishi wa wachungaji mmoja ambaye ni Mch. Mwiligumo, wawakilishi wa wakristo
Ndg F. Phiri na Joseph Kajinga, OCD na Mkuu wa Upelelezi (DCI), katika
mazungumzo ya upatanishi muafaka ukakubalika kwa pamoja kuwa kamati tendaji
ikaitishe Halmashauri kuu ya jimbo ili iitishe Sinodi. Askofu Alinikisa Cheyo mbele ya
Halmashauri kuu alikataa kuitisha Sinodi na kuwaambia wajumbe kuwa Mkuu wa
Wilaya alikuwa anawaburuza tu. Kwa mara ya pili tena Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
alikutana na kamati tendaji, katika mazungumzo hayo muafaka ukawa jibu sahihi
ni Sinodi na mapatano yakawa baada ya Pasaka
mwezi wa nne kuanzia tarehe 1/05/2014 mpaka tarehe 30/06/2014 muwe mmeitisha
Sinodi Askofu hakuwepo. Tarehe 13/05/2014 walipoita Bodi, bado Askofu alisikika
akisema Sinodi haitaitwa mpaka Sinodi ya mwaka 2016. Mkuu wa Wilaya hawezi
kutuamulia mambo yetu, wakati huo huo anaenda Shirikani kufanya uchochezi kwa
kumtangaza Mch. B. Buya kuwa ni mwizi na kumchafua zaidi kwa mfano:-
- Alikwenda Ushirika wa Ruanda mbele ya Ibada na
kusema Mch. N. Buya amekula Tshs 600,800,000/= (millioni mita sita la laki nane) na kuwauliza
wakristo Je tumrudishe tena Mch. N. Buya mbadhilifu na ninyi ni watoaji
wazuri?, hatuwezi kumrudisha Buya. Hii inaonyesha ni uchochezi wa hali ya juu.
- Pia alikwenda Makongolosi Chunya nako amesema
hayo hayo, kaenda Mtaa wa Songwe alikuwa anaanza kusema hivyo hivyo na
alipomuona Mch. N. Buya anaingia
Kanisani akabadilisha usemi, kuwa sisemi Mch. N. Buya amekula hizo pesa
.
Hivyo baada ya
mchanganuo huu Ushirika wa Bethlehemu tunatoa tamko lifuatalo
- Askofu Alinikisa Cheyo ajiuzuru wadhifa wake wa Uaskofu mara moja kwa kukiuka na kuilinda Katiba ya
Kanisa la MORAVIAN TANZANIA JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI Ibara ya 33:i pia kukiuka
wajibu wake kama Askofu kama inavyoelekezwa IBARA 33, Kifungu cha B, Kipengele
i, ii, iii, na iv kwa kuacha huduma ya Kiaskofu na kujitwalia madaraka ya
kiutendaji na kuendelea kufanya uchochezi kwenye Shirika mbalimbali
anazotembelea.
TAMKO HILI LIMETAMKWA NA BARAZA LA WAZEE
USHIRIKA WA BETHLEHEMU
……………………………………………… …………………………………………
MWANDISHI WA BARAZA MWENYEKITI WA BARAZA
LA WAZEE -
BETHLEHEMU LA WAZEEE, USHIRIKA WA
BETHLEHEMU







Post a Comment