![]() |
| Ofisa wa mifumo ya kibenki ya kielektroniki, Kalington Chahe, toka benki ya CRDB akizungumza katika semina hiyo |
![]() |
| Ofisa wa mifumo ya kibenki ya kielektroniki, Kalington Chahe, toka benki ya CRDB akiwaonyesha washiriki wa Semina hiyo namna mfumo huo unavyotumika |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF pamoja na Benki ya CRDB
wametoa mafunzo ya matumizi ya tiketi za
elektroniki mkoani Mbeya kwa kushirikisha
wasimamizi wa mechi katika uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine mbeya , viongozi
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA).
Wengine waliopatiwa mafunzo hayo , meneja wa Uwanja wa Sokoine na
msaidizi wake, makatibu wa Tanzania Prisons na Mbeya City, maofisa habari wa
Mbeya City na Tanzania Prisons, Ofisa Usalama wa MREFA na wasimamizi wa
milangoni (stewards).
Semina hiyo inalengo la
kuwanda wadau hao katika kusimamia
mfumohuo utakao anza na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na
Tanzania Prisons kwa mchezo wao wa kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza katika
semina hiyo Ofisa wa mifumo ya kibenki ya kielektroniki, Kalington Chahe, toka benki ya CRDB, mfumo huo unatoa fursa kwa
kila mtu kupata fursa ya kutazama mechi pasipo kuwa na usumbufu wa aina yoyote
katika hususani katika suala la ununuzi a tiketi.
Amesema kwa kila mtu
mwenye simu ya mkoni anauwezo wa kununua tiketi hata tano kwa wakati mmoja na
kuepuka suala la kulanguliwa na mawakala wasio waaminifu.
“Tumefanya hivyo
makusudi kwa kuwa tunaamini kuwa katika familia baba anaweza kununua tiketi
tano ambazo ataingia yeye na familia yake isiyozidi watu wane, hivyo kufanya
idadi ya watu kutoka familia moja kuwa watano” alifafanua Chahe.
Hata hivyo amesema kuwa
hali hiyo haizuii timu kununulia mashabiki wake tiketi za mchezo kwani kutakuwa
na utaratibu wake.
Akichangia mada katika
mafunzo hayo, mmoja wa washiriki , Charles Mwakipesile, alitoa changamoto juu
ya mfumo huo utakavyowezesha timu za majeshi zinazokuwa na mashabiki wake
maalumu ambao mara nyingi huingia bure uwanjani.
Mechi hiyo ambayo
itakuwa ya kwanza kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa matumizi ya tiketi za
elektroniki kwa washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili jioni.
Kiingilio ni sh. 3,000
kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo (Julai Mosi mwaka huu).
Wakati huo huo, Afisa
Habari wa TFF Boniface Wambura amesema kutakuwa na utaratibu maalumu kwa waandishi wa
habari za michezo kwa ajili ya kuripoti mechi hiyo.
mwisho













Post a Comment