Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Meneja kituo cha Uwekezaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Daud Riganda akizungumza katika moja ya moja mikutano ya uwekezaji  jijini Mbeya

NaEmanuelMadafa,Mbeya
Hatua ya Halmashauri mbalimbali Mikoa ya Kanda za Nyanda za juu kusini kushindwa ku tenga maeneo maalumu kwa ajili ya uwekezaji kumechangia kwa kiwango kikubwa kudhorotesha sekta hiyo ya uwekezaji katika ukanda huo.
 
Aidha hatua hiyo pia imekuwa ikisababisha pia kuibuka kwa migogoro  ya mara kwa mara baina ya wananchi na wawekezaji  katika maeneo husika.
 
Akizungumza jijini Mbeya  Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda za nyanda (TIC) Ndugu ,Daudi Riganda amesema kuwa kukosekana kwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji imekuwa changamoto kubwa kwa wawekezaji hali ambayo imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa kudhorotesha sekta hiyo.
 
 
Amesema katika Mikoa mingini ya ukanda huo   haina maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ardhi  ya wawekezaji licha ya serikali kulipia kelele suala hilo.
 
 Aidha amebainisha kuwa endapo Wawekezaji watapewa maeneo ambayo yamepimwa kuna uwezekano mkubwa migogoro mikubwa ambayo inasababishwa na hali hiyo ikapungua na hata kukoma kabisa.
 
Akizungumzia kuhusu uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya ,Riganda amesema kuwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya wamekuwa wana fedha nyingi lakini cha ajabu wamekuwa wagumu kuwekeza kwenye vitu vikubwa ambavyo vinaweza kuwa msaada kwa baadaye.
 
Amesema kuwa badala yake fedha hizo wamekuwa wakitumia kwenye nchi za China kufanya biashara  mbali mbali huku wakishindwa kufikiria vitu vya msingi vya kuwekeza.
 
Aidha Meneja huyo wa Kanda amesema kuwa Agosti mosi mwaka huu wanategemea kuwa na kongamano la siku tatu ambalo lengo lake ni kuibua vivutio vya uwekezaji  katika mikoa ya Mbeya, Iringa,Njombe na kwamba Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu ,Mizengo Pinda .
 
Hata hivyo amesema wageni wengine ambao wanatarajiwa kuwepo katika kongamano hilo mabalozi 16 kutoka nchi mbali mbali  .
 
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top