Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Makachero wa jeshi la Polisi wakiwa wamebeba sanduku lenye madawa ya kulevya wakitoa katika mahakama kuu tayari kwaajili ya kuyateketeza.



Makachero wakipakia masanduku yenye madawa ya kulevya katika gari la Polisi.


Masanduku yenye Madawa ya kulevya yakiwa tayari kwaajili ya kuteketezwa


Moto Mkubwa ambao umetumika kwaajili ya kuteketeza Madawa ya kulevya.Picha na David Nyembe


Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Nyanda za Juu Kusini, imetoa amri ya kuteketeza moto dawa za kulevya aina ya Heroin zikiwa na uzito wa Kilogram 34.664 zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8 baada ya upande wa mashitaka kufunga kusikiliza utetezi wa shauri hilo.

Dawa hizo, zilikamatwa mwaka 2010, katika eneo la Tunduma mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Zambia zilidaiwa kusafirishwa na raia wawili kutoka nchini Afrika Kusini, Vuyo Jack (33) pamoja na mkewe Anastazia Elizabeth.

Akitoa amri hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania (Mbeya) Noel Chocha, alisema mahakama baada ya kumaliza kutumia vielelezo hivyo kwenye kesi hiyo ya usafirishaji wa dawa za kulevya ikiwa ni kinyume cha sheria sura ya 16 kifungu kidogo (i)(b)(i) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 inaamuru kuteketezwa moto dawa hizo ndani ya saa moja mara baada ya kuhairisha kusikiliza shauri hilo.

Awali, mahakama hiyo ilishindwa kuteketeza vielelezo hivyo kutokana na mshitakiwa Vuyo Jack kuiomba mahakama kuvitumia vielelezo hivyo wakati wa utetezi wa kesi yake ambao umemalizika juzi.

Mahakama hiyo, mara baada ya kufunga kusikiliza utetezi wa mshitakiwa huyo wa kwanza ilitoa nafasi kwa mshitakiwa wa pili Anastazia Elizabeth, endapo nayeye angependa kutumia vielezo hivyo kwenye utetezi wake unaotarajia kuanza, Julai 28 mwaka huu ambaye alikataa kwa kuimbia mahakama ya kwamba hatavitumia.

“Hivyo kutokana na mshitakiwa wa pili kukataa kutumia vielelezo hivi kwenye utetezi wake ni vema vikateketezwa kwa kuchomwa moto ndani ya saa moja mara baada ya kuhairisha shauri hili,”alisema Jaji Chocha.

Aidha, dawa hizo zikiwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi zilitolewa ndani ya mahakama na kusafirishwa mpaka kwenye eneo la tukio ambako wahusika walikamilisha taratibu za uchomaji wa dawa hizo za kulevya kisha kuziteketeza kwa kuzichoma moto.


Dawa hizo aina ya Heroin ziliteketezwa kwa moto wa nyuzi joto 700 hadi 900 huku wahusika wote wakishuhudia kukamilika kwa zoezi hilo, vikiwemo vyombo vya dola, waandishi wa habari, baadhi ya wanachi wa eneo hilo na washitakiwa wenyewe.

Ili, kufahamu ya kwamba zoezi hilo limefanyika vizuri bila ya kuacha shaka miongoni mwa watu, wahusika walipatiwa elimu kutoka kwa wataalamu kwa kueleza alama za rangi ya moto itakayoonekama wakati wa zoezi hilo likifanyika.
.

Hata hivyo zoezi la uchomaji lilianza kwa mtaalamu kutupia pakti moja moja ndani ya moto huo ukiwa na nyuzi joto kati ya 700 na 900 mpka vifurushi vyote 37 vilipomalizika.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top