Na EmanuelMadafa,Mbeya
Timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na Tanzania
Prisons zinacheza mechi ya kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza
kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kwa
washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili jioni.
Kiingilio ni sh. 3,000 kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza
kuuzwa leo (Julai Mosi mwaka huu).
Wakati huo huo, keshokutwa (Julai 3 mwaka
huu) kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki yatakayofanyika
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuanzia saa 3 asubuhi.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa
mechi katika uwanja huo, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya
(MREFA), meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake, makatibu wa Tanzania
Prisons na Mbeya City, maofisa habari wa Mbeya City na Tanzania Prisons, Ofisa
Usalama wa MREFA na wasimamizi wa milangoni (stewards).







Post a Comment