Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na EmanuelMadafa
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 4-2 na wenyeji, Botswana leo mjini Gaborone katika mchezo nwa kirafiki. Mabao ya Stars yalifungwa na Khamis Mcha 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' kwa penalti
Mechi imefanyika katika  Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
mwisho



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top