Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Mkuu  Mheshimiwa Mizengo Pinda akifungua kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya Iringa ,Njombe na Mbeya katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa jijini Mbeya kongamano ambalo limehudhuriwa na vingozi mbalimbali wa serikali katika mikoa hiyo pamoja na taasisi binafsi na wadau mbalimbali . 
Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu (uwekezaji na uwezeshaji)  Daktari Mary Nagu akizungumza katika kongamano hilo 
Mmoja wa wadau wakubwa katika sekta ya uwekezaji wa pili kulia Mzee Mzindakaya akiwa makinini kufuatilia yanayojili katika kongamano hilo




Mkuu wa Mkoa wa mbeya Abbas Kandoro akitoa salama za Mkoa  katika Kongamano hilo 




Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christina Ishengoma akitoa salama za Mkoa wa Iringa katika kongamano hilo 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wawekezaji waliohudhuria Kongamano hilo katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya.
Picha ya pamoja ya Waziri Mkuu na Viongozi mbalimbali 
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ametoa saa 12 kwa uongozi wa Shirika hodhi la mashirika ya umma nchini (CHC) kufika mkoani Mbeya, ili kumpatia sababu zilizosababisha kushindwa kupatikana kwa mwekezaji katika kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeya.

Waziri Pinda ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya  wakati wa kongamano la uwekezaji la kanda ya nyanda za juu kusini,kwa kummuagiza Waziri wa  nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk. Mary Nagu, baada ya viongozi wa shirika hilo kukosekana ukumbini ili kutoa maelezo.
Kutokana hali hiyo, alimtaka Dk. Nagu kuwasiliana na wawe wamefika mkoani humo leo  jioni ili  wakutane naye na kumpatia maelezo ya kina juu ya sababu zinazosababisha kukosekana kwa mwek,ezaji katika kiwanda hicho.

Waziri Mkuu Pinda yupo mkoani humo kwa ziara ya ya kikazi ya siku mbili, ambapo leo  amefunghua kongamano hilo la uwekezaji na kesho  anatarajia kuzindua maonesho ya wakulima ya Nanenane  kwa mikoa hiyo.

Agizo hilo la Pinda kufufuliwa  kwa kiwanda hicho ni la pili, ambapo mwaka 2011 alipofanya ziara mkoani hapa, alitoa miezi 6 kwa viongozi wa CHC wahakikishe wampata mwekezaji na kiwanda hicho kuanza kazi.

Akiwahutubia wadau hao wa sekta ya uwekezaji , Waziri Mkuu Pinda alisema mikoa ya Nyanda za juu kusini ina fursa kubwa katika sekta hiyo tena kwa kuwatumia wawekezaji wa ndani.

Pinda amesema kufufuliwa kwa kiwanda hicho kitawanufaisha wananchi wengi , hususani vijana kupata ajira.

Aidha, Waziri pinda, alishangazwa na kitendo cha watendaji wa shirika hilo kutohudhuria kongamano hilo ambalo linanafasi kubwa ya kutoa fursa kwa wewekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza hali itakayosaidia kukua kwa uchumi na maendeleo kupatikana.

Kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeya ni miongoni mwa viwanda kadhaa vilivyokufa na kusababisha tatizo kubwa la ajira hususani kundi la vijana.

Akitoa maelezo katika ziara ya  awali ya Pinda mkoani hapa, mwaka 2011, ofisa wa kiwanda chja nyama Mbeya, Joseph Mapunda, alisema ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mwaka 1975 na ulikamilika na kuanza kazi mwaka 1985 .
Mwisho.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top