NA MWANDISHI WETU, TANGA.
TIMU
ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” kesho Jumapili
itacheza
mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani
ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara
ambao unatarajiwa kuanza Septemba 20 hapa nchini.
Akizungumza
leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
maandalizi
ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na tayari
walishafanya
mazungumzo na uongozi wa wakata miwa hao hivyo watawasili
mkoani
hapa siku moja kabla ya mchezo huo.
Assenga
amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa timu ya Coastal
Union
kucheza ikiwa mkoani hapa baada ya kurejea kutoka Visiwani Pemba
ilipokuwa
imeweka kambi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matayarisho ya
ligi
kuu soka Tanzania bara.
Amesema
baada ya mchezo wa kwanza timu hiyo kuibuka na ushindi wa
mabao
2-0 dhidi ya Polisi Morogoro hivyo waliona umuhimu wa mechi hiyo
lengo
likiwa kukipa makali kikosi hicho kabla ya kuwavaa wekundu wa
msimbazi
Simba siku ya ufunguzi wa Ligi kuu.
Ameongeza
kuwa wanategemea mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa sana
hivyo
wakazi wa Tanga na vitongoji vyake watumia fursa hii kuja kuiona
timu
yao ya Coastal Union ikipambana kwenye mchezo huo kabla haijaanza
msimu
mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Hata
hivyo amesema kuwa msimu huu timu hiyo imepania kuhakikisha
inafanya
vizuri katika mechi zake za nyumbani na ugenini ili kuweza
kuchukua
ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara .
Post a Comment