Mkutano
kati ya waandishi habari na Waathirika wa Mabomu Mbagala, ambao umefanyika
katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu ,jijini Dar-Es-Salaam mapema leo
.
Waathirika hao wapatao 1,361 kati yao 25 wameishapoteza maisha
kutokana na athari za mabomu hayo.
Mlipuko huo wa mabomu ni tukio lililotokea tarehe 29 April mwaka
2009,majira ya saa sita kasa robo katika eneo la mbagala kuu,hii ni baada ya
mabomu hayo kulipuka katika ghala la silaha ya kambi ya ulinzi ya jeshi ya
jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) namba 671 kj.
Mabomu hayo yaliyokua yanalipuka kwa mfululizo yalisababisha
vifo,kujeruhi,kuharibu makaazi na mali za watu kuharibiwa vibaya na kwa upande
wa afya athari zilizojitokeza ni maradhi ya TB ama kifua kikuu,upofu wa
macho,saratani,tezi yamkojo na kadhalika.
Leo hii wananchi wanadai kua serikali imewasahau na kuwatelekeza
waathirika hao kiasi cha huduma za afya kukosekana,malazi kutorejea kama
walivyoahidiwa na kila walipodai fidia wanapata majibu yasiyo faa ikiwemo,
wanaoweza kusubiri wasubiri ama wasio kua na subira basi wajitoe.CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment