Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi Mussa Husein wa kwanza kushoto akitoa rariba nzima ya Serengeti Fiesta katika mahojiano yake ndani ya Generation Fm Mbeya katika kipindi kinachoendeshwa na Twali B |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Kwa mwaka 2014 hakika wakazi wa
jiji la mbeya na vitongoji vyake utakuwa
ni mwaka wa kihistoria kwao kutokana na
kufunguliwa tena kwa pazia la burudani
yanii Serengeti Fiesta 2014 nisheedah ikihusisha burudani mbalimbali
kama Serengeti Soka Bonanza pamoja na Serengeti Diva Supar Nyota bila kuwasahau
wazee wa fursa.
Mmoja wa waraatibu wa shughuli
nzima ya Serengeti Fiesta 2014 kwa Mkoa wa Mbeya Bw.Mussa Hussein amesema tayari
kwa kiwango kikubwa maandalizi ya burudani hizo zimefikia katika hatua nzuri
ambapo kwa sasa burudani hizo zimeanza na hatua ya utoaji wa zawadi kwa wadau
ambao wamekuwa wakishiriki moja kwa moja katika mchakato huo wa serengetoi
fiesta 2014 jijini hapa.
Akitoa ratiba nzima ya Sherehe
hizo Mussa amesema septemba 26 mwaka huu kutakuwa na Bonanza litakalo husisha timu
4 kutoka katika bar mbalimbali za jiji la Mbeya ambapo mshindi wa kwanza katika bonanza hilo
atapatiwa zawadi ya Katoni kumi za bia kutoka Serengeti huku mshindi wa pili
akipatiwa katoni 5 bonanza ambalo litafanyika katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu( T.I.A ). jijini hapa.
Amesema bonanza hilo lifanyika kwa lengo la kuamsha hisia za wakazi
wa jiji la mbeya katika kuelekea kilele cha Serengeti Fiesta 2014 katika
viwanja vya Sokoine siku ya jumapili Septemba 28 mwaka huu.
Aidha Mratibu huyo amesema mara
baada ya kukamilika kwa Fiesta Soka Bonanza kutakuwa Serengeti Pree Party siku ya jumamosi Septemba 27 itakayo fanyika katika ukumbi wa Babiz Cafee ambayo itahudhiriwa ana wasanii
mbalimbali watakao pata fursa ya kupafom katika show ya Serengeti Fiesta
Sokoine kwa kiingilio cha shilingi 10000.
Amesema Septemba 28 mwaka huu
majira ya saa 4 asabuhi kutakuwa na Serengeti Diva supar Nyota ndani ya ukumbi
huo wa Babiz ambapo baadaye majira ya saa 8 mchana kutakuwa na semina za fursa
katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa semina ambazo zitaongozwa na Bw.Luge pamoja
na wadau mbalimbali.
Hata hivyo Bw.Mussa ametoa wito
kwa wakazi wa jiji hilo kujitokeza kwa wingi katika kilele cha burudani hizo
huku akiwataka wakazi hao kuondoa hofu juu ya kuwepo kwa uharibifu wa uwanja wa
sokonie kwani burudani nzima hazita husika katika eneo la pichi la uwanja huo
hasa kutokana na kuwepo kwa ulinzi mkali pamona eneo zima kuzungushiwa kamba
ili kuzuia kabisa uhalibifu wa uwanja huo
Mwisho.
Post a Comment