Waandishi wakiwa makini kufuatilia mkutano huo |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Katika kuhakikisha serikali
inatimiza azma yake ya kuwakomboa wakulima nchini hususani katika suala la
kilimo bora cha kibiashara taasisi binafsi
zinazojiuhusisha na shughuli ya usambazaji wa mbegu bora za kilimo zimeendelea na harakati
za kuisaidia serikali katika suala hilo.
Hatua hiyo ni pamoja na
kutoa elimu pamoja na kusambaza pembejeo bora za kilimo zenye kukidhi mahitaji
ya mkulima.
Kutokana na hali hiyo
kampuni ya Seed Co imezindua
shindano rasmi la mashamba darasa kwa shule za Msingi Tanzania ambazo zitaanza mchakato
wa kulima shamba darasa kwa kufuata
kanuni bora za kilimo cha kisasa .
Akizungumza jijini Mbeya
Kaimu meneja wa Kampuni hiyo Kanda ya Nyanda za juu Kusini Ndugu Michael
Rikanga amesema shindano hilo ni
mahususi kwa shule za msingi za Mbeya
Iringa Njombe na Ruvuma pamoja na Rukwa na Katavi ambapo shindano hilo
linatalajiwa kuanza msimu mpya wa kilimo .
Amesema kwa shule
itakayokuwa imelima shamba darasa zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo
bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati yenye thamani ya shilingi
mili15.
Amesema pamoja na zawadi hiyo ya madati kwa mshindi wa kwanza
pia mshindi atapatiwa sare za
michezo madaftari na kalamu za kuandikia
pamoja na mwalimu wa somo la kilimo kupatiwa simu ya mkononi.
Amesema ili kushiriki
mwanafunzi au mwalimu wanatakiwa kutembelea maduka ya mawaka maalum
waliothibitishwa na Kampuni hiyo ya Seed Co ili kujisajili katika shindano
hilo.
Hata hivyo Meneja huyo
amesema kuwa katika hatua za uandaaji na usimamizi wa shamba darasa Kampuni
hiyo itatoa pemebejeo zote zitakazohitajika
ikiwa ni pamoja na mbegu za mahindi mbolea ya kupandia na kukuzia .
Mahitaji mengine ni pamoja na madawa ya kupulizia
iwapo iwapo mazao yataonyesha dalili za kushambuliwa na wadudu waharibifu.
Lengo la kampeni hiyo
kufundisha kilimo kwa njia ya
vitendo kwa wanafunzi wa shule za msingi sanjali na kutoa nafasi kwa wanafunzi kujishindia zwadi kutoka
katika kampuni hiyo ya Seed Co Tanzania Limited.
Mwisho.
Post a Comment