Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Godfrey Zambi.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
SERIKALI inatarajia kununua tani 200,000 za mahindi,
huku ikifanya jitihada za kutafuta masoko zaidi nje ya nchi ili kuhakikisha
wakulima wote wanauza kwa tija.
Kauli
hiyo imetolewa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Godfrey Zambi, wakati wa ziara yake
ya kikazi ya kutembelea vituo vya wakala wa hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA)
Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Amesema,
lengo la serikali ni kuhakikisha inanunua mazao yote ya mahindi kutoka kwa
wakulima hivyo mbali ya kuchukua tani hizo pia inaendelea na mikakati ya
kutafuta masoko ya nje ili kuhakikisha wakulima wanauza zao hilo kwa faida.
Amesema
licha ya serikali kutokuwa na uwezo wa
kuchukua mahindi yote yaliyopo mikononi mwa wakulima nchini, bado inaendelea na
jitihada za kutafuta masoko nje ya nchi.
Amesema,
wakulima wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanahifadhi mahindi ili yawe na
ubora utakaolingana na bei inayotolewa, lakini pia kuvutia masoko ya nje ya
kimataifa).
Aidha,
Zambi, amewataka wakulima hao kutokubali kurubuniwa na wachuuzi ambao hivi sasa
wananunua bei ya mahindi kwa shilingi 5000 hadi 6000 kwa debe wakati serikali
inanunua mahindi hayo kwa shilingi 9000 kwa debe, bei ambayo haiwezi kupatikana
katika soko lingine ndani na nje ya nchi.
Aidha,
kwa upande wake,Meneja Kanda ya Makambako wa NFRA, Abdulahi Nyangasa, amewataka
watendaji na watumishi wa wakala, kuhakikisha wanakagua mizigo yote ya mahindi
ambayo inawaslishwa kwenye vituo hivyo, huku akiwasisistiza wakulima
kuhakikisha wanachambua mahindi kabla ya kuyafikisha vituoni.
Aidha
amesema wakala hao wa hifadhi ya taifa ya chakula mwaka jana ilinunua zaidi ya
tani 16000 za nafaka katika kituo cha Mbozi, ambapo mwaka huu inatarajia
kununua zaidi ya tani 15000.
Mwisho
|
Post a Comment