KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI |
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA
GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA
WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.497
AFR AINA YA MITSUBISHI CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SEFANIA MSIGALA (40) MKAZI WA MABADAGA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WALIOFARIKI NI PAMOJA NA DEREVA WA GARI HILO AITWAYE SEFANIA MSIGALA NA ABIRIA AITWAYE RIZIKI MHANGA (45) MKAZI WA NJOMBE. AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.09.2014 MAJIRA YA SAA 04:15 ALFAJIRI KWENYE MTEREMKO HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ITEWE, KATA YA ITEWE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA
VIJIJI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PASTON MAJUTO (09) MKAZI WA INYALA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.481 ABF
AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE KUDRA BAKARI (44) MKAZI WA SOWETO JIJINI MBEYA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.09.2014 MAJIRA YA SAA
09:20 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA INYALA, KATA YA INYALA, TARAFA YA
TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA
ZA MISAKO:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA INYASI SAKAYA (28) MKAZI WA MAJENGO – MAKONGOLOSI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI MISOKOTO
MIWILI [02].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.09.2014 MAJIRA YA SAA
05:30 ALFAJIRI HUKO STAND YA MAGARI – MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI,
TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA ALIKUTWA AKIWA ANAVUTA BHANGI HIYO NA
ALIPOPEKULIWA ALIKUTWA NA MISOKOTO HIYO MIWILI KWENYE MFUKO WAKE WA SURUALI.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment