Mwekezaji wa ndani katika Sekta ya Kilimo, Hamis Msigwa, ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Kilimo ya young Masitus Enterprises Ltd . |
Bw.Msigwa akiwa shambani kwake Kapunga Rice Project Chimala Mbarali Mbeya. |
Mifereji ya maji inayotumiwa na mwekezaji huyo katika kilimo cha mpunga eneo la Kapunga Chimala Mkoani Mbeya |
Moja ya Malori yakipakia mpunga kutoka kwa mwekezaji huyo ambao unasafilishwa kwenda sokoni. |
Magunia ya mpunga yakisubili kupakiwa kwa ajili ya kuingia sokoni . |
Bw. Msigwa akiwa kazini kukatua mashamba kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo |
Shamba la Mzee Msigwa likiwa teyari kwa ajili kupandwa mbegu ya mpunga . |
Wafanyakazi wa Kampuni ya young Masitus Enterprises wakipakia mbegu katika mshine maalumu kwa ajili ya upandaji |
Na EmanuelMadafa,mbeya
SERIKALI imeshauriwa kuweka mfumo utakaowabana Wawekezaji hasa wa
Sekta ya Kilimo nchini kuwa Wawezeshaji wa Teknolojia kwa Wakulima Wadogo ili
kuwa na Taifa lenye Wakulima wenye uwezo wa kuzalisha mazao kwa viwango vya Kimataifa.
Serikali imetakiwa kutambua kuwa ili Uwekezaji katika Sekta ya
Kilimo uwe na faida kwa Taifa ni lazima Wawekezaji wanaokuja nchini watumike
kama chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kitaaluma kwa Wakulima wa Tanzania
badala ya kulipa kodi na kuchangia huduma za kijamii pekee.
Ushauri huo kwa Serikali umetolewa na Mwekezaji wa ndani katika
Sekta ya Kilimo, Hamis Msigwa, ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Kilimo ya young
Masitus Enterprises Ltd katika mahojiano maalum shambani kwake eneo la Kapunga,
Chimala wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Msigwa amesema Serikali inapaswa kuweka mfumo utakaowalazimisha
Wawekezaji wa Kilimo kushirikiana na wakulima wadogo katika shughuli zao na
kuwapa mbinu za kilimo bora kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuinua
uzalishaji wao.
Amesema mfumo wa sasa unaowaruhusu wawekezaji kuwatumia watanzania
kama vibarua wa miradi yao hauwezi kuwa na faida kwa Taifa kwa sababu hautoi
fursa nzuri kwao kujifunza teknolojia mpya zinazotumiwa na wawekezaji hao.
Msigwa ambaye katika eneo hilo la Kapunga anamiliki ekari 1,365 za
mashamaba ya mpunga, amesema kitu kinachotakiwa ni kwa wawekezaji hao kuwa
mteja wa wakuliwa wazawa ambapo wanatakiwa kuwawezesha kiteknolojia na pembejeo
huku wakiwhakikisha wanakuwa wanunuzi wa mazao yatakayozalishwa na wakulima hao
ili kuwawezesha kunufaika na kilimo hicho.
Alisema hatua hiyo pia itamrahisishia mwekezaji husika katika
upatikanaji wa nguvu kazi ya mradi wake kupitia mfumo ambao utaboresha
mahusiano baina yake ya wananchi wanaozunguuka eneo lake la uwekezaji.
Hata hivyo, Msigwa, amesema ili Tanzania ifikie lengo la mapinduzi
ya Kilimo ni lazima Wakulima nchini wazingatie ushauri wa kitaalam badala ya
kulima kwa mazoea ambapo wanatakiwa kuwatumia Maafisa Ugani waliopo kwenye
maeneo yao ili kuzalisha mazao kwa viwango vya ubora unaotakiwa.
Sekta ya kilimo inahusisha zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania
hivyo uwekezaji makini unahitajika katika sekta hiyo.
Mwisho
Post a Comment