Afisa Habari na Mahusiano Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Boniface Wambura |
Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ngao
ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga
itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ni sh. 5,000.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na
kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu
vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.
Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za
elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti
vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.
Wakati huo huo Mwamuzi wa daraja la kwanza
(class one), Luteni Godwill David Lugenge aliyefariki dunia juzi (Septemba 7
mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ameagwa leo
(Septemba 9 mwaka huu).
Luteni Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani
ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Ligi Kuu, akiwa na ndugu yake Christopher
Alexander Lunyungu katika gari dogo walipata ajali hiyo wakati wakienda mkoani
Kilimanjaro.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ambalo limetoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kwenye
shughuli ya kuaga itawakilishwa na mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Saloum Umande Chama.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu
Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake
lihimidiwe
mwisho
Post a Comment