Na EmanuelMadafa,Mbeya
KIKONGWE cha miaka 70,
kimeuawa kwa kupigwa risasi aina ya SMG maeneo ya mkono wa kushoto chini ya
bega na kupelekea kifo chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo limetokea jana, majira ya saa tisa
za usiku katika eneo la Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya.
Amemtaja marehemu huyo
kuwa ni Nkusubila Kaminyonge (70) mkazi wa eneo la Soweto lililopo Jijini
Mbeya.
Akielezea tukio
hilo, Kamanda Msangi, alisema inadaiwa kuwa wauaji hao, walivunja geti la
nyumba ya marehemu huyo kisha kuingia ndani na kutekeleza unyama huo.
“Inadaiwa kuwa, watu hao
walivunja geti la nyumba na kisha kuingia ndani na kuvunja mlango wa chumba
alichokuwa amelala marehemu na kumpiga risasi”alisema Msangi.
Amesema, kuwa wakati
watu hao wakifanya unyama huo, imeelezwa kwamba marehemu alikuwa amelala ndani
na mume wake aitwaye Osia Malambugi(72) mkazi wa Soweto Jijini Mbeya.
Amesema, kwa mujibu wa
maelezo kutoka kwa mzee huyo, inadaiwa kuwa mara tu ya watu hao kufyatua risasi
mzee huyo alishtuka baada ya kusikia mlio mkubwa wa risasi na kukuta mke wake
amepigwa.
Aidha, Msangi, amefafanua
kuwa, inasemekana kwamba wauaji hao mara baada ya kufanya tukio hilo
walifanikiwa kukimbia.
Hata hivyo, amesema kuwa
uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu hao hawakuchukua kitu chochote na kwamba
askari wanaendelea na upelelezi wa mauaji hayo.
Mwisho.
Post a Comment