Meneja masoko Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Evance Mwakyusa akimkabidhi zawadi mshindi wa shindano hilo Ndugu Jumma Seleman Mkazi wa Sumbawanga Mkoani Rukwa. |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
KAMPUNI ya New Habari
2006 Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The
African, jana ilimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi Juma Selemani 22,
baada ya kushinda shindano la Twenzetu Brazil kushuhudia mechi ya Kombe la
Dunia.
Mshindi huyo ni muongoni
mwa washindi wanne waliojishindia simu ya Smartphone ikiwa na muda wa maongezi
kutoka Kampuni ya Tigo wa shilingi 120,000, lakini yeye alishindwa kukabidhiwa
zawadi hiyo kwa muda muafaka kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Kampuni.
Akimkabidhi zawadi hiyo
jana, Meneja masoko Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Evance Mwakyusa, alisema
shindano hilo lilikuwa likiendeshwa kupitia magazeti ya Bingwa na Dimba,
mshindi huyo alipatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyofanyika katika Ofisi za
New Habari, Sinza, Kijiweni.
Amesema, kampeni hiyo
ilidumu kwa muda wa miezi miwili na kushirikisha wasomaji wa Bingwa na Dimba
kwa kutuma kuponi zilizopo kwenye magazeti hayo.
Amesema, Juma Selemani
ni miongoni mwa washindi wengine wanne ambao walifanikiwa kujinyakulia zawadi
ya simu ya mkononi lakini mshindi huyo hakuweza kukabidhiwa zawadi yake
kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Kampuni.
Akizungumza , mara ya kukabidhiwa simu hiyo, Juma, alitoa pongezi kwa uongozi wa
Kampuni hiyo kwa kuchezesha shindano hilo, ambalo limemuwezesha kujipatia simu
ya smartphone baada ya kununua magazeti 10 ambayo sawa na shilingi 8000 ya
kitanzania.
Alisema, kushiriki
shindano hilo ilikuwa ni mara yake ya kwanza na kwamba aliweza kutuma kuponi 10
kwa awamu mbili ndani ya mwezi mmoja na kuibuka mshindi wa simu hiyo.
Kampuni ya New Habari
(2006) Limited, iliandaa shindano hilo ili kuwapa fursa Watanzania kuweza
kushiriki na watu wengine duniani furaha ya mchezo wa soka, unaochezwa na
kupendwa na watu wengi duniani kwa kwenda Brazil au kuangalia kupitia luninga
watakazoshinda.
Aidha shindano hilo
lililenga kuwapa hamasa vijana wa kike na wa kiume kushiriki katika mchezo wa
mpira wa miguu, kupitia Kombe la Dunia ambalo ni tukio kubwa la kimichezo
linalotokea kila baada ya miaka minne.
Mwisho.
Post a Comment