Mkurugenzi shirika la Nyumba Nchini (NHC) Neemia Mchechu |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Jumla
ya shilingi Milioni 31.5 zimetolewa na shirika la Nyumba Nchini (NHC), kwa
ajili ya matengezo ukarabati wa madarasa manne ya shule
ya Msingi ya Hasanga iliyopo Jijini Mbeya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo
Neemia Msechu, akikabdhi msaada huo mbele ya mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu Abbas
Kandoro ame sema ukarabati huo ni moja ya miakakati iliyojiwekea shirika hilo
katika kuhakikisha llinarudisha fadhila kwa jamii.
Amesema,
jamii imekuwa na mchango mkubwa kwa shirika hilo kutokana na kodi wanazolipa
kupitia majengo yao ya makazi na ofisi wanazopangisha hivyo ni vema nao
wakarudisha shukrani kwa jamii kwa kupitia njia hiyo.
Amesema
katika jengo la utawala ukarabati uliofanywa ulihusu uezuaji wa paa, ujenzi
mpya wa kuta za jingo, bimu, upigaji lipu na upakaji wa rangi, pamoja na
uwekaji wa milango ya kisasa na yenye hadhi ya aluminium, uliogharimu sh. Mil
22,774,900.
.Hata
hivyo, Msechu amesema kuwa Shirika hilo lipo kwenye makakati wa kujenga
nyumba za gharama nafuu katika eneo la Songwe lililopo Mbeya Vijijini
baada ya halmashauri hiyo kutoa eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 290.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbasi Kandoro, aliitaka jamii kuthamini michango
inayotolewa na wahisani, hususani wale wa ndani ili kuwashawishi zaidi katika
kufanikisha michakato mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
Awali
akisoma risala, mmoja wa walimu wa shule hiyo,Neema Sanga, alisema shule hiyo
iliyojengwa mwaka 1975 ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo
uchakavu wa
mwisho
Post a Comment