Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, AHMED Z. MSANGI – SACP
anawatangazia Wananchi wote ya kuwa vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka
2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi
la Polisi, Usaili huo utafanyika kuanzia Tarehe 28.09.2014 hadi Tarehe
01.10.2014 kuanzia majira ya saa 08:00 Asubuhi hadi saa 16:00
jioni katika Shule ya Sekondari Mbeya Day.
Muhimu:
·
Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya
masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)],
nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo
cha kuzaliwa haitakubalika.
·
Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo
atachaguliwa.
·
Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri,
chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu
za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia tarehe
ya usaili na muda wa kuanza usaili.
Post a Comment