Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Mkuu wa Uingereza Davd Cameroon
Nchini Uingereza imefahamika kwamba vifaa vyote vya kisasa vinavyotumika majumbani vyenye uwezo wa kuunganishwa kwenye mtandao wa internet vitawekewa vizuizi vya picha za ngono ama pengine familia ziamue kupokea picha hizo zitaachwa zijimalize zenyewe na watoto wao,hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Uingereza ,David Cameron.
Kwa kuongezea,waziri mkuu wa Uingereza ,kuzuia picha za ngono mtandaoni na ubakaji vitakua ni kinyume cha sharia kwa England na Wales na baadaye itafuatia Scotland.
Bwana Cameron ametoa onyo hilo wakati alipokua anatoa hotuba yake kuhusiana na ngono mtandaoni na kueleza kua kunadumaza watoto na utoto na akaeleza kua wateja wa sasa na wapya watahusika na sharia hiyo mpya.
Onyo hilo la waziri mkuu wa Uingereza linakuja miaka saba baadaye wakati ambapo David Cameroon aliwahi kuwaambia Google kwenye mkutano kwamba wanasiasa wanapaswa kushawishi makampuni kubadilisha na sio kubadili sharia hizo.
Na leo ametangaza kwamba amefanikiwa kufikia makubaliano na makampuni makubwa manne juu ya kuweka chujio la picha za ngono,baada ya matukio ya nyuma ya pazia kua na sehemu kama hizo.
Pia akadokeza kua endapo makampuni makubwa kama google hawatakubaliana na wito huo wa kuzuia masharti ya utafutaji ,atatunga sheria.CHANZO BBC


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top