Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na Mwandishi wetu,Tanga
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kufanya
utambulisho rasmi kwa wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu
mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotazamiwa kuanza kutimua
vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Utambulisho huo utafanyika siku ya “Coastal Union day” ambayo
hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7 mwaka huu ambao kufanyika
mchezo wa mpira wa miguu ambapo msimu huu Coastal Union itacheza na
Polisi Morogoro kwenye uwanja CCM Mkwakwani.

Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya
kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa .

Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo
wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya
mazungumzo kumalizika.

Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza
kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze
kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania
bara

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu,Assenga
amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji
kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top