Baadhi ya wanafunzi wakiwa na walimu wao wakijaribu kupata ufafanuzi toka kwa uongozi wa chuo hicho. |
Mazungumzo yakiendelea ndani ya ukumbi na uongozi wa chuo hicho |
Picha na Davd Nyembe wa Fahari News
Na Mwandishi wetu,Mbeya
WANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi cha Kanisa la Moravian, Jimbo la Kusini
Magharibi, wamegoma na kutishia kukatisha masomo yao kwa kile wanachokidai
kuchoshwa na kauli za fedheha na matusi zinazotolewa na
Mkuu wao wa chuo hasa pale wanapodai haki
zao za msingi.
Tuhuma hizo ambazo ziliambatana na vurugu za kutishia kuzivunja
ofisi za chuo hicho huku baadhi yao wakilizunguka eneo hilo, wakimsubili Mkuu
wa chuo hicho, God Lwinga kutoka nje kwa madai ya kumshushia kipondo.
Vurugu hizo zilianza majira ya asubuhi, ambapo wanachuo hao,
wapatao 83 wa kozi za umeme, ushonaji na ufundi selemala,
walilizingira eneo la geti kwa lengo la kuzuia gari la kiongozi
huyo, ili asitoke nje kisha kutimiza lengo lao.
Wakati, wanachuo hao wakiendelea na jaribio hilo, inasemekana Mkuu
huyo wa chuo alitoa taarifa polisi ya kuomba msaada, ambapo askari polisi
walifika na kufanikiwa kutuliza vurugu hizo ikiwa na kunusuru
kichapo alichokusudiwa kupewa kiongozi huyo.
Wakizungumza kwenye mkutano wa makubaliano ulioitishwa
na na uongozi wa chuo hicho kwa kushirikisha viongozi wa jeshi la polisi,
Wanafunzi hao, walisema kuwa Mwalimu Mkuu huyo, amejenga tabia ya
kuwadharau kwa kutoa lugha za matusi na kejeli pale wanapofikisha
matatizo yao.
Wamesema, Mwaka jana, uongozi wa chuo uliwasilisha mfumo upya wa
ufundishaji wa masomo chuoni hapo kutokana na uongozi wa Veta kutoa mtaala mpya
wa kufundishia ambao umeweka bayana kwamba wanafunzi watahitajika kusoma miaka
mitatu badala ya miwili ili kupata cheti kinachotambulika na
serikali.
Wamesema, hivyo wao kama walengwa amabao walitakiwa kumaliza elimu
hiyo mwaka huu kabla ya mabadiliko hayo walimfuata kiongozi huyo kwa lengo la
kuwasilisha maoni yao kutokana na changamoto zinazowakabili, jambo
ambalo limeonekana kuwa kero kwa Mkuu huyo wa chuo hivyo kudaiwa kutumia lugha
hizo za matusi ambazo zimeonekana kuwakera wanafunzi hao.
Akijibu malalamiko hayo ya wanafunzi, Mkuu wa Chuo hicho, God
Lwinga, alisema yeye hakubaliani na tuhuma zinazotolewa na wanafunzi
hao kwani uongozi wa chuo ulishawaeleza kila kitu na wao walikuwa wanaufahamu
mkakati huo wa Veta.
Hata hivyo, Mkuu huyo aliwataka wanafunzi hao walio na utayari wa
kuendelea na masomo kuandika barua na watakao ona elimu waliyoipata inawatosha
basi wanaweza kuendelea na shughuli zao za kutafuta maisha kupitia ujunzi huo
walioupata.
Mwisho.
Post a Comment