Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abas Kandoro

Na Mwandishi wetu,mbeya
 Katika kuhakikisha vitendo vya ajali za barabarani vinapungua na kukoma kabisa serikali Mkoani Mbeya imeanzisha mpango kabambe utakao saidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hilo.

Hatua hiyo ni pamoja na kunyang’anywa leseni kwa Madereva wote wa mabasi ya abiria watakaobainika kusababisha ajali kwa uzembe.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akizungumza na abiria, madereva na mawakala wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya mkoa huo na mikoa mingine nchini leo alfajili jijini hapa amesema uchunguzi uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi  na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, SUMATRA, umebaini kuwa ajali nyingi za barabarani zinasababishwa na mwendo kasi kutokana na madereva wanaotaka sifa za kuwahi kufika safari zao.

Amesema, licha ya juhudi kubwa zinzofanywa na mamlaka husika katika kukabiliana na ongezeko la ajali nchini lakini juhudi hizo zinakwamishwa na madereva wenye tabia ya kuendesha mabasi kwa mwendo kasi hivyo Serikali mkoani Mbeya imeamua kuwadhibiti madereva hao.

Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa ametangaza rasmi kwa hautua ya utekelezaji wa  kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafutia leseni zao ili kuwaondoa kabisa kwenye sekta hiyoya usafirishaji.

Mbali na madereva hao, Kandoro pia amewataka abiria kuacha tabia ya kuwachochea na kuwafurahia madereva wanaoendesha magari kwa mwendo kasi kwani tabia hiyo ni miongoni mwa sababu za ajali nchini.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, SACP Ahmed Msangi, amesema watasimamia agizo hilo ili kuhakikisha lengo la kukabiliana na ajali za barabarani mkoani hapa linatekelezwa ipasavyo.

Amesema, ajali za barabarani kwa nkoa wa Mbeya, zimeongezeka kwa kasi kubwa kutoka January mwaka huu hadi mwezi Septembar jumla ya ajali 297 zimetokea huku vifo vya watu vikiwa ni 210.

Aidha, Kamanda Msangi, amewataka mawakala wa mabasi hayo kuacha tabia ya kutoa motisha kwa madereva wa magari yanayowahi kufika kwani hicho ndicho chanzo cha ajali.

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top