Na Emanuel Madafa,Mbeya
Kufuatia kuwepo kwa ongezeko
la ajali za barabarani nchini hususani kwa Mkoa wa Mbeya Mamlaka ya Udhibiti
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, SUMATRA Mkoani Mbeya imesitisha leseni za
mabasi ya kampuni tano za usafirishaji wa abiria mkoani hapa yakiwemo mabasi ya
Super Feo kutokana na kukiuka sheria za barabarani.
Kaimu
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Denis Daud, alisema
Super Feo imesitishiwa leseni za mabasi yake kuanzia Septemba 11 mwaka huu.
Amesema hali hiyo ni kutokana na basi lake lenye namba za usajili T
273 CDD lililokuwa likitokea Songea kwenda Mbeya kupata ajali katika eneo la
Sanangura Songea na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 24 kutokana na
mwendo kasi.
Amesema,
kwa mujibu wa taarifa za awali za uchunguzi, kutoka Jeshi la Polisi, chanzo cha
ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi uliosababisha kugonga mti na kupinduka.
Amebainisha
kuwa kwa kuzingatia kifungu namba 15 cha sheria ya SUMATRA na pia kanuni namba
22 ya kanuni za ufundi, Usalama na Ubora wa Huduma za Mwaka 2008, Mamlaka
inasitisha lesseni ya usafirishaji kwa mabasi ya Kampuni ya Super Feo kutoa
huduma katika njia zote Tanzania tarehe 11/9/2014.
Amesema,
mabasi hayo ambayo yanamilikiwa na mmiliki Moses Amlani, hayataruhusiwa
kujishughuisha na shughuli zozote zile za usafirishaji mpaka hapo,
muhusika atakapotekeleza baadhi ya masharti yaliyopendekezwa na mamlaka hiyo.
Aidha,
Daudi, amesema kuwa moja ya masharti ambayo mmiliki atatakiwa kuyatekeleza ni
pamoja na kuwasilisha vyeti vya mafunzo ya kuendesha abiria(PSV) vya madereva
wake pamoja na kujaribiwa na jeshi la polisi kwa lengo la kujiridhisha kama
wana sifa za kuendesha mabasi.
Amesema,
lingine ni mmiliki kuwasilisha na kukaguliwa na SUMATRA mikataba ya ajira ya
madereva wote wa kampuni yake pamoja na kadi za uanachama wa mifuko ya pensheni.
Pia,
SUMATRA imesitisha leseni za mabasi manne yanayosafirisha abiria kati ya Mbeya
Mjini na Ubaruku wilayani Mbarali kutokana na kushiriki katika mgomo kwa
kufunga barabara ili kuzuia shughuli za usafirishaji kwa lengo la kushinikiza
madai yao kwa Serikali.
Amesema,
kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni Na. 18(i) (b) na 32 (1) (h) ya kanuni za
leseni za usafirishaji(Magari ya abiria) 2007 na kupitia kifungu Na. 15 cha
sheria ya SUMATRA, mamlaka imeamua kusitisha leseni zao na kwamba wahusika hao
hawatajihusisha kutoa huduma ya usafirishaji.
Aliyataja
magari hayo kuwa ni Coaster yenye namba T423 BSA ambayo inafanya shughuli zake
za kusafirisha abiria Mbeya- Rujewa, Coaster T339 safari za Mbeya- Rujewa,
Coaster namba T640 BAN pamoja na Fuso namba T968.
Hata
hivyo, Afisa huyo, aliwataka madereva na wamiliki wa magari kuzingatia sheria
na kanuni za utoaji wa huduma kwa jamii kwani mamlaka haitasita kuwachukulia
hatua watu watakao kuka taratibu hizo ili iwe fundisho pamoja na kupunguza
idadi ya vifo vya watu vinavyotokana na uzembe.
Post a Comment