Na Gwamaka Mwankota,Mbeya
Timu ya soka ya Mbeya city jumamosi hii
inataraji kucheza mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Vipers
Fc zamani bunamwanya inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uganda mchezo
utakaopigwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya.
Akiongea na kipindi hiki afisa habari
wa Mbeya City Dismas Ten amesema kuwa kikosi hicho kinataraji kutua jijini
Mbeya ijumaa ya kesho kikiwa na msafara wa watu 25 viongozi 5 na wachezaji 20.
Ten ameongeza kuwa timu hiyo ianataraji
kuwa kipimo kizuri kwa timu ya Mbeya City kwani mmoja ya timu amabazo
zimeonyesha uwezo mkubwa katika ligi ya Uganda na kufanikiwa kushika nafasi ya
nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo.
Huu utakuwa mchezo wa mwisho wa
kujipama nguvu kwa Mbeya City kabla kuanza mbilinge la ligi kuu ya soka
Tanzania bara inayotaraji kuanza kutimua vumbi September 20 kwenye viwanja
mbalimbali.
Mbeya city ambayo ilikamata nafasi ya
tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea na mawindo
yake chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi na msaidizi wake Suleiman Jabir
Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten
amewaomba wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo jumapili
kuishuhudia timu yao pendwa ikionyesha kile ambacho imejipanga nacho kwa ajili
ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015.
mwisho
Post a Comment