Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mkazi wa Upendo Wilayani Chunya Mkoani mbeya Ndugu  Mahoma Salasini (30)  auawa kwa kuchomwa kisu katika sikio la kulia na katika shavu lake la kulia na mtu aliyefahamika kwa jina la Godfrey Lams (30) mkazi wa mbuyuni – chunya.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 09:00 huko katika kitongoji cha mbuyuni “b”, kata ya mbuyuni,  wilayani  chunya, mkoani wa mbeya.

Chanzo cha mauaji ni wivu wa kimapenzi, kwani inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja aitwaye melenia mgata (24) mkazi wa mbuyuni ambaye awali alikuwa na uhusiano na mtuhumiwa na baadae waliaachana/walitengana.

Mtuhumiwa amekamatwa. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa mbeya linawashikilia watu wawili ambao ni  Six Manam (22) na Noram Marcus (20) wote raia na wakazi wa nchini ethiopia wakiwa wameingia nchini bila kibali/kinyume cha sheria.

Wahamiaji hao haramu walikamatwa mnamoOctoba   06 mwaka huu  majira ya saa 01:00 usiku baada ya kufanyika msako ulioshirikisha askari polisi wa tanzania na nakonde nchini zambia katika maeneo ya mwaka, kata  ya Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani  mbeya.

Taratibu za kuwakabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea.
Mwisho.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top