Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 12 yatafanyika Desemba mwaka huu jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa kutangaza mpango wa
programu ya vijana inayolenga Fainali za Afrika za U17 mwaka 2019 ambapo
Tanzania imeomba kuwa mwenyeji, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema mashindano
hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote.
Mashindano hayo yatafanyika kuanzia
Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza,
Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350.
Rais Malinzi aliwashukuru wakurugenzi wa
shule za Alliance (James Bwire) na Lord Baden Powell (Kanali mstaafu Idd
Kipingu) kwa kukubali shule zao kuwa za kwanza kuanzia programu hiyo ya vijana.
Pia aliishukuru kampuni ya Symbion ambayo
imetoa sh. milioni 100 kwa ajili ya kuunga mkono mashindano hayo ya U12.
Symbion ni moja ya wadau wanaoshirikiana na TFF katika mpango wa miaka mitano
ya programu za vijana.
Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall
aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo ambayo imeambatanishwa
(attached).
Post a Comment