Hatua
hiyo imefikiwa baada ya kura za ndio zilizopigwa na wajumbe kufikia kiwango
kinachostahili.
Ili
katiba hiyo iliyopendekezwa ipite ilitakiwa kuungwa mkono na kura za ndio
theluthi mbili kutoka Tanzania bara na theluthi mbili za ndio kutoka Zanzibar.
Jumla
ya wajumbe wote wa bunge hilo la Katiba ni 629, huku 419 wakitoka Tanzania bara
na 210 kutoka Zanzibar.
Zoezi
hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo
yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi
ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.
Kabla
ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum la katiba lilikaa kama kamati
kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya
Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.
Baada
ya kamati hizo za bunge hilo kutoa mapendekezo yao, kamati ya uandishi ilikuwa
na jukumu la kuandika upya Ibara za Sura za Rasimu ya Katiba zilizojadiliwa na
Bunge Maalum na hatimaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti baada ya kukamilisha kazi
hiyo.
Hivyo,
Kamati ya Uandishi ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mapendekezo ya
marekebisho, maboresho au mabadiliko katika Rasimu ya Katiba yanakidhi matakwa
na masharti ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014.
Hatma
ya katiba hiyo itahitimishwa kwa kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa na
wananchi.CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment