Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bi.Grace Mugabe kulia
Mwandishi aliyeshinda tuzo nchini Zimbabwe Chenjarai Hove amemtaka Grace Mugabe mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kurudisha shahada ya uzamifu aliyopewa.
Alipewa shahada hiyo na chuo kikuu cha Zimbabwe mwezi uliopita.
Lakini kumekuwa na lalama kuhusu mda aliyochukua katika chuo hicho kusomea shahada hiyo,huku baadhi ya duru zikiarifu kuwa alichukua miezi miwili pekee na sasa wanafunzi wanataka swala hilo kuchunguzwa.
Hatahivyo chuo hicho hakijatoa tamko lolote kuhusu mgogoro huo.
''Hatua hiyo inaathiri uadilifu wa kitaalam'', bwana Hove aliiambia BBC.
Shahada aliyopewa si ile ya heshima bali ni ya kusomea taaluma fulani,alisema mwandishi huyo.
Hove aliyehitimu kutoka chuo hicho cha Zimbabwe amesema kuwa alimwandikia Naibu Chansela wa chuo hicho akimtaka kuelezea hatua hiyo.
Katika barua aliomwandikia mkuu huyo, Hove amesema kuwa chuo hicho kimepoteza heshima yake kwa kuwa shahada za chuo hicho sasa hazina maana.
Matamshi yake yanajiri huku muungano wa wanafunzi wa taifa hilo ukiandaa kuwasilisha kesi mahakamani siku ya Alhamisi ukitaka chuo hicho cha Zimbabwe kutoa maelezo kuhusu vile mke huyo wa rais alivyopata shahada hiyo.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top