Mwalimu wa shule ya Msingi Ruiwa Wilayani Mbarali mkoani mbeya Ndugu Laiton Ngoli akiwa na wanafunzi wake ambao ni watoto wa jamii ya wafugaji. |
Masomo yakiendelea |
Nje ya Darasa |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Serikali ya Kijiji cha Maendeleo Kata ya
Ruiwa Wilayani Mbarali Mkoani kwa
kushirikiana na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Ruiwa,Manfred komba, waamua kuanzisha shule ya msingi kinyume
cha utaratibu, lengo likiwa ni kujitafutia kipato kutoka kwa wafugaji.
Aidha shule hiyo inavyumba viwili vya kufundishia pamoja na ofisi
moja ya walimu imejengwa kwenye Kijiji cha Maendeleo kilichopo katika Kata ya
Ruiwa na kwamba inajumla ya wanafunzi 320 kuanzia ngazi ya awali hadi darasa la
sita.
Pia, watoto hao hufundishwa na Mwalimu mmoja aliyetambulika kwa
jina la Laiton Ngoli ambaye aliwekwa na wananchi wa eneo hilo ambao ni jamii ya
wafugaji kuwafundisha wanafunzi ngazi ya awali kutokana na shule zilizopo
kujengwa mbali hivyo kuwalazimu watoto kutembea umbali mrefu wa kilomita 11 -8.
Wakizungumza na blog hii, wananchi wa kijiji hicho cha Maendeleo,
walisema kutokana na jiographia ya eneo hilo kuwa mbaya hasa nyakati za
mvua, iliwalazimu wao kujenga majengo hayo mawili , kisha kumuomba Mwalimu
Laitoni Ngoli kuwafundisha watoto wao elimu ya awali.
Wamedai kuwa wakati Mwalimu
huyo akiendelea kutoa elimu hiyo ya awali, inasemekana Mwalimu Mkuu wa shule ya
Msingi ya Ruiwa Manfred Komba kwa kushirikiana na watendaji wa serikali ngazi
ya Kata na Mratibu wa elimu Kata, Joseph Mrita, walifika na wazo nzuri la
kumtaka mwalimu huyo kufundisha watoto wa darasa la kwanza hadi la
sita ingawa watoto wa darasa la nne na la sita
wamesajiliwa shule ya msingi mama ya Ruiwa.
Amesema, hali hiyo imewatia mashaka na kubaini kwamba viongozi hao
wamekuwa wakiwachezea mchezo kwa kuchukua fedha zao ambapo inasemekana kuwa
kila mfugaji amekuwa akichangia kiasi cha fedha thamani yake ikiwa
ni ng’ombe wawili hadi watatu.
Mbali, na changamoto hizo, pia wazazi hao wamehoji ubora
wa elimu inayotelewa na mwalimu huyo ambaye inasemekana hajakidhi
vigezo vya kufundisha madarasa ya juu.
Akizungumzia hilo, Mwalimu Laiton Ngoli,
alikiri serikali ya kijiji kumpa dhamana ya kufundisha watoto hao
licha ya kutambua kiwango chake cha taaluma kinaishia wapi, huku akisisistiza
kwamba ameanza kufundisha darasa la kwanza na sita mwaka 2010
hadi hivi sasa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya msingi ya Ruiwa,
alikiri Mwalimu huyo kufundisha watoto hao lakini aligoma kuzungumzia suala la
usajili wa shule hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Maendeleo Charles Mkisi
alisema serikali ilitoa kibali cha wazazi kuongeza majengo
ya madarasa ya kusomea watoto kwenye eneo hilo lakini suala la
usajili halifahamu.
Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya ya Mbarali, Enerico Batinaluho
, alisema suala hilo ndio analisikia kutoka kwa waandishi wa habari na
kuhaidi kulifuatilia.
Hata hivyo, wazazi hao wameiomba Serikali kuingilia kati hatma ya
shule ya Msingi ya Kijiji hicho kwani msimu wa mvua umekaribia hofu
yao kubwa ni ufikaji shuleni kwa watoto hao ambapo licha ya kutembea umbali
mrefu bado itawalazimu kuvuka mito mikubwa miwili ya maji.
Mwisho.
Post a Comment