Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Vijana wa Mbeya City fc 

Katibu wa Mbeya City Fc Emanuel Kimbe akiangusha sahihi yake mbele ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tanzania, Basil Gadzios, wakwanza Kushoto. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mbeya City fc Bw.Mapunda akiangusha sahihi yake 

Asanteni sana




Katibu wa Mbeya City akitoa zawadi kwa uongozi wa Cocacola 
Na EmanuelMadafa,Mbeya

TIMU ya Mbeya City inayoshiriki Ligi kuu Tanzania bara , imeendelea kushukiwa na neema baada ya Kampuni ya Vinywaji baridi Coca Cola, kuingia mkataba wa miaka miwili  ukiwa na thamani ya shilingi milioni 150.

Akisaini Mkataba huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tanzania, Basil Gadzios, amesema kampuni hiyo imeidhamini Timu ya Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili na kwamba fedha hizo zitatolewa kwa awamu mbili.

Amesema, lengo la kudhamini timu hiyo ni kurudisha fadhila kwa watanzania ambao wamekuwa mstali wa mbele kutumia bidhaa zinazozaliwa na kampuni hiyo.

 Akizungumzia Mkataba huo, Katibu wa timu ya Mbeya City, Emanuel Kimbe, amesema Kamupuni ya Coca Cola, imeingia udhamini na clabu hiyo wa miaka miwili na kwamba fedha hizo zitatolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza kampuni itatoa milioni 75 na awamu ya pili itamaliza kwa kutoa milioni 75 lakini baadhi ya fedha hizo zitatolewa kwa njia ya vinywaji.

Amesema, uongozi wa kampuni utatoa kiasi cha fedha taslimu cha shilingi milioni 60 huku milioni 15 zitaingizwa kwenye gharama za vinywaji vitakavyokuwa vikitolewa na kampuni kwenye klabu hiyo katika kipindi chote cha udhamini.

Aidha,amesema, klabu hiyo inatarajia kuongeza nembo kwenye jezi zao ambapo muda si mrefu  jezi hizo zitakuwa zikionekana tofauti kidogo.

Amesema hatua ya Cocacola kuidhamini timu hiyo ni faraja kubwa kwa uongoiz wa timu hiyo pamoja na wachezaji wenyewe kwani campuni hiyo ni moja ya kampuni kubwa duniani hivyo hatua hiyo itasaidia pia kuitangaza timu hiyo ndani na nje ya Tanzania

Hata hivyo, Kimbe, alitumia nafasi hiyo kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kutokata tamaa haraka kutokana na timu hiyo kuanza vibaya kwani uongozi unafanya mabadiliko ya kiufundi kwa wachezaji wake.

Pamoja na kusainiwa kwa mkataba huo pia katibu huyo  amewataka mashabiki wasikate tama kutokana na timu yao kuto anza vyema msimu wa ligi hivyo   uongozi unafanya utaratibu wa kuibadilisha timu hiyo kiufundi hivyo muda si mrefu Mbeya City ya zamani itarudi kwenye mstari wake.

Aidha Kimbe amesema licha ya mapungufu hayo madogomadogo  bado vijana wake wanaonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu ili kuwaridhisha mashabiki wao hasa kutokana na kiingilio wanachotoa ..

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top