Jenerali
Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali
Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya
kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali
Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la
maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Waandamanaji
walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore
wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu
kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali
Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha
wabunge .
Runinga
ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika
la utangazaji.
Waandamanaji
kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile
baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati
mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege
ukifungwa.
Rais
Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge
wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore
kuwania tena Urais mwaka ujao.
Watu watano wameuawa
katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa
Blaise Compaore.
Awali
wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore
alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua
akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa
na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania
tena.BBC SWAHILI
Post a Comment