Habari kubwa weekend hii ni ile ya kukamatwa kwa Chidi Benz akiwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akisafiri kuelekea Mbeya.
Rapper huyo mwenye kipaji, alikamatwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi na hadi sasa anashikiliwa na polisi.
Muimbaji wa muziki, Rehema Chalamika aka Ray C amempa pole msanii huyoa ambaye miezi kadhaa iliyopita alidaiwa kumpiga. Ray C amesema hana kinyongo naye na amempa ushauri muhimu.
“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja. Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta litakuwa kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya,” ameandika Ray C kwenye Instagram.
“Kama mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na unazuilika na kutibika,ana kipaji na ana uwezo wa kurudi tena kwenye sanaa,tumuombee mema. Tanzania Stand Up n Wish Him Luck…………With Love,Ray C Foundation,” aliongeza
Post a Comment