Mwenyekiti
wa zamani wa Simba SC, Ismail Aden Rage amekanusha tetesi kuwa amekuwa
akiihujumu timu hiyo ili ifanye vibaya kwenye mechi zake. Kupitia
Kikaangoni Live ya EATV, Rage alisema akiwa kama shabiki mkubwa wa Simba
aliyoitumikia kwa muda mrefu, hawezi ili ipate matokeo mabovu.
“Kusema
kweli siwezi kuihujumu timu yangu Simba nadhani mimi nimeitumikia kuliko watu
wengine wengi tu hapa na pia hapa nilipofika kwa sasa Simba wana mchango wao
mkubwa tu hivyo siwezi kuihujumu Simba,ila nachoweza kusema ni kwamba mashabiki
pamoja na uongozi wa Simba uliopo madarakani sasa katika mpira kuna mambo
matatu kushinda sare au kufungwa kwa hiyo tukubali haya matokeo,pia tuwape muda
huenda timu ikabadilika mbele ya safari,” alisema.
Hivi
karibuni Simba iliwasimamisha wachezaji wake watatu, Shabani Kisiga, Amri
Kiemba na Haruna Chanongo kutokana na kudaiwa kuchangia matokeo mabovu ya timu
hiyo.
Hata hivyo Rage alisema hafikirii kugombea nafasi yoyote kwenye
klabu hiyo. “Sijafikiri kugombea nafasi ya Rais katika Klabu ya Simba
kwani nahitaji kupumzika,sasa hivi uongozi wa simba ni mgumu sana,” alisema.
Post a Comment