Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jijini mbeya Ndugu Samuel Bubelwa akionyesha moja vifaa vinavyo tumika kwa ajili ya kuhamasisha wananchi juu usafi wa mazingira. |
Taka zikiwa zimekusanywa kwa ajili ya kubebwa na gari la jiji ambapo mfuo huo umenzishwa ili kuondokana na tatizo la uchafua katika maeneo ya madambo katika maeneo ya makazi ya watu |
Wakazi wa uyole utukuyuni jijini mbeya wakipakia taka ndani ya gari la jiji . |
Halmashauri ya jiji la mbeya kwa sasa lipo katika kuhakikisha
linakabiliana na tatizo la kudhibiti uchafuzi
wa mazingira na kuboresha usafi wa mazingira kwa kuwashirikisha
wadau mbalimbali waliopo ndani na nje
jiji la mbeya.
Makusudi ya kuwashirikisha
wadau mbalimbali ni katika kutumia rasilimali zilizopo kwa kuongeza uwezo wa jiji kugharamia usafi wa mazingira kwa njia
shirikishi na kwa kutumia viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya mtaa kata na Halmashauri.
Akizungumzia mikakati hiyo mkuu wa idara ya usafishaji na
mazingira jijini mbeya ndugu Samuel Bubelwa amesema katika kuhakikisha mikakati hiyo inafanikiwa eneo la jiji la mbeya
limegawanywa katika kanda tano za
usimamizi wa usafi wa mazingira ili kuwa
na eneo dogo la usimamizi ambalo litashirikisha ipasavyo uongozi wa mtaa na
kata.
Amesema kwa muda mrefu
huduma za usafi na utoaji taka zimekuwa
zikitolewa kwa jamii bila malipo ya
uchangiaji hali ambayo imepelekea wananchi
kuona kuwa kazi ya usafi wa
mazingira ni ya jiji pekee .
Amesema hali hiyo kwa kiwango kikubwa imedhohofisha mfumo mzima wa usafi na uzoaji taka hasa kutokana na wananchi wenyewe kuwa ndio
chanzo cha uchafuzi kuto shirikishwa
katika kugharamia usafi.
Kutokana na hali hiyo Bubelwa amesema mipango ya huduma endelevu
imekuwa inaelekezwa kwa wananchi juu ya
suala la uchangiaji wa gharama za uendeshaji
kwa kulipia tuzo kiasi ili kusaidia serikali kutoa huduma iliyo bora
kama ilivyo katika uchangia wa
sekta ya elimu.
Mwisho.
Post a Comment