Mgombea wa nafasi ya Ukatibu wa Chadema mbeya Ndugu Fanuel Mkisi ambaye fomu yake ilipotea kabla ya muda wa kuomba kura. |
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Mbeya kimefanya uchaguzi wa kumpata Katibu wa chama hicho mkoani mbeya ambapo uchaguzi huo ulighubikwa na mizengwe pamoja vituko vya aina yake.
Hatua hiyo ni pamoja
na mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo fomu yake kupotea katika mazingira ya kutatanisha kabla
ya kuanza kwa mchajakato wa kujieleza kwa wagombea wote na kuomba kura kutoka
kwa wajumbe.
Taarifa ya kupotea kwa
fomu hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya Joseph
China,licha ya jina la mgombea huyo kuwepo katika orodha ya wanaowania nafasi
hiyo.
Mwenyekiti huyo
alimwita mgombea wa nafasi hiyo ndugu Fanuel Mkisi kwa lengo la kutaka
kufahamu kuwa fomu hiyo aliikabidhi kwa nani, ndipo alipoeleza
kuwa kwamba fomu hiyo alimkabidhi kiongozi red Briget Jamali Juma na
kwamba sababu za kufanya hivyo ni kutokana na Mwenyekiti aliyepaswa kuzipokea
fomu hizo kuwa na mazungumzo na mmoja wa mgombea mwenza.
Hata hivyo, baadhi ya
wajumbe walilaani kitendo hicho na wengine kuwatuhumu baadhi ya viongozi
kuhusika na tukio hilo, lengo likiwa ni kumbeba mgombea huyo kwa kumtafutia
kura za huruma kutoka kwa wajumbe hao.
Wamesema kitendo cha kupotea kwa fomu ya mgombea huyo ilitakiwa pia hata uchaguzi wenye uhalishwe lakini chaa ajabu uchaguzi huo ulifanyika licha ya kuwepo kwa kasoro hiyo
Kitendo cha kushangaza
zaidi ni pale uchaguzi ulipomalizika na Mwenyekiti China, kukutana Mwandishi
wa blog hii kueleza kuwa fomu ya mgombea
huyo imepatikana na kwamba ilikuwa imejichanganya na makaratasi mengine
yaliyokuwa kwenye meza kuu.
Uchaguzi huo
ulifanyika katika ukumbi wa "King Leaders Hotel" uliopo ndani ya Kata
ya Nsalaga- Uyole Jijini Mbeya ambapo mchuano ulikuwa baina ya
wagombea watatu.
Wagombea hao ni Boyid
Mwabulanga aliyekuwa akiitetea nafasi hiyo Fanuel Mkisi pamoja
na Jidawaya Kazamoyo.
Hata hivyo, uchaguzi
huo ulifanyika kwa awamu mbili kutokana na matokeo ya awamu ya kwanza ya
wagombea wawili kugongana kwa kupata kura 14 huku mgombea watatu ambaye ni
Jidawaya akipata kura 12 kati ya 41 zilizopigwa huku kura moja ikiharibika.
Kutokana na matokeo
hayo, Msimamizi wa uchaguzi,Janson Gwilugumo ambaye ni Mwenyekiti Chadema ni
msingi Kanda ya Nyanda za Juu kusini, aliomba muongozo kutoka kwa wajumbe baada
ya matokeo hayo kutokidhi vigezo vya uchaguzi kwa kutofikisha asilimia 50 kama
Katiba inavyoelekeza.
Baada ya kupendekeza
ombi hilo, baadhi ya wajumbe walipendekeza kufanyika duru la pili kwa wagombea
hao wawili kwani lengo ni kufikia asilimia 50 inayotakiwa na Chadema.
Mapendekezo hayo
yaliungwa mkono na wajumbe wa baraza la mashauriano na hatimaye uchaguzi
ulifanyika kwa mara ya pili na mgombea Boyid Mwabulanga aliibuka mshindi kwa kupata
kura 21 dhidi ya 19 alizopata Mkisi kati ya kura 40 zilizopigwa baada ya mpiga
kura mmoja kuomba udhuru.
Hata hivyo mara baada
ya uchaguzi huo kumalizika mmoja wa wagombea pamoja na wajumbe wa mkutano huo
walieleza kuwa kitendo cha kupotea kwa fomu ya mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo
ni moja ya mikakati ya kumebeba mgombea huyo.
Walisema pamoja na mkakati huo kukwama bado kuna dalili kubwa ya
mgombea huyo kuchukua nafasi hiyo ya ukatibu kewani majina yote yanapekekwa
makao makuu ya chama hicho ambapo kati ya maina hayo moja wapo linaweza
kupitishwa na kuwa katibu hata kama kura zake hazikutosha.
Mwisho
Ndugu Jidawaya Kazamoyo akiomba kura kwa wajumbe |
sasa hapa tunafanye wajemeni mambo ena ndo hivyo tena |
Mgombea nafasi ya ukatibu Boidi Mwabulango akiomba kura kwa wajumbe |
Post a Comment