WATU watatu wanaosadikiwa ni majambazi, wanashikiliwa na polisi Mkoani Mbeya, kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha ikiwemo wizi wa pikipiki.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo
limetokea jana majira ya saa 12:00 jioni katika eneo la Sokoine lililopo Jijini
Mbeya.
Aliwataja, majambazi hao kuwa ni Joseph Kigali(24)
mkazi wa Madabaga Wilayani Mbarali, Juma Nelsoni na Emmanuel Mwakaja
mkazi wa eneo la Pambogo Jijini Mbeya na kwamba watu hao walikutwa
na pikipiki moja, vifaa vya pikipiki , silaha aina ya Shot Gun, risasi saba,
visu na nondo.
Akielezea tukio hilo, Msangi alisema kuwa watuhumiwa wawili ambao
ni Joseph Kigali na Juma Nelsoni, walikamatwa ndani ya uwanja wa Sokoine wakati
mechi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar ikicheza.
Alisema, inasemekana kwamba watuhumiwa hao walifanikiwa kuiba
pikipiki ya Alfonce Gabriel ambayo alikuwa ameiegesha nje ya uwanja wa Sokoine
wakati akiangalia mechi hiyo iliyokuwa ikiendelea uwanjani.
Alisema, kwa mujibu wa maelezo ya Alfonce, inasemekana kwamba
vijana hao walianza kumfuatilia wakati akitoka nyumbani hivyo aliingia mashaka
na o na kuweka mitego iliyofanikisha kutiwa nguvuni.
Alisema, mechi ilipomalizika mmiliki huyo, alifika katika eneo
aliloegesha mali yake hiyo na kutofanikiwa kuiona ndipo alipoanza kuingiwa
mashaka na wale vijana na kuanza mchakato wa kuwatafuta na kufanikiwa
kuwakamata.
Alisema, vijana hao walipohojiwa na polisi walifanikiwa kumtaja
kiongozi wao ambaye ni Emmanuel Mwakaja na kuwapeleka askari eneo
alipojihifadhi jambazi huyo na kufanikiwa kumtia nguvuni.
Hata hivyo, Kamanda Msangi, alisema kuwa watuhumiwa
hao,walipopekuliwa walikutwa na visu, nondo, mapanga,pikipiki moja, silaha aina
ya Shot Gun pamoja na risasi saba.
Mwisho.
Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi |
Post a Comment