Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Nouman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo katika kituo cha Afya Mwanjelwa jijini hapa. |
Dkt Sigalla akitoa chanjo wa mmoja wa watoto kama sehemu ya uzinduzi wa Chanjo hiyo |
Mwakilishi wa Jambo leo Ndugu Venance Matinya akijianda kupatiwa chanjo. |
Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga |
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Mussa Zungiza |
Kampeni
ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imezunduliwa rasmi leo jijini Mbeya ambapo kimkoa kampeni hiyo imefanyika Wilayani Ileje mkoani hapa.
Pia kampeni hiyo itawahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 15.
Aidha kampeni hiyo itaambatana na utoaji wa matone ya Vitamini
A, dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi,Matende na
Mabusha.
Pia lengo na madhumuni ya
kampeni hiyo ni kudhibiti milipuko ya magonjwa ya Surua na Rubella ili
kupunguza vifo na madhara yanayosababishwa na magonjwa hayo..
Chanjo ya Surua na Rubella itatoa fursa ya kutoa kinga kwa
watoto wengi zaidi ambao hawakupata chanjo hiyo utotoni katika mikoa yenye
maambukizi makubwa ya magonjwa hayo ambayo ni Mtwara, Lindi, Tanga ,
Dar es salaam,Morogoro, Pwani, Tabora, Manyara, Iringa, Ruvuma,
Rukwa, Katavi, Singida, Dodoma na Njombe.
Surua na Rubella
itatolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka 15, matone ya
vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi chini ya miaka 5.
Nyingine ni dawa za minyoo (Mebendazole) zitakazotolewa kwa
watoto wenye umri wa miezi 12 hadi chini ya miaka 5 nchi nzima na dawa za
kutibu na kukinga minyoo (Albendazole) Usubi, Matende na mabusha au Ngirimaji
kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea katika mikoa 16
iliyobainishwa.
Katika uzinduzi huo wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao
katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo hiyo.
Pia ametolewa wito kwa mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanapata
chanjo ya Surua-Rubella ili kuwakinga watoto wao dhidi ya matatizo ya Moyo,
mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na mtindio wa ubongo yanayotokana
na ugonjwa huo.
Mwisho.
Post a Comment