Kamara
alirudi nchini Ugiriki baada ya kuichezea timu ya taifa lake Sierra leone
katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya taifa bora barani Afrika dhidi ya
Cameroon.Kilabu hiyo ilimwambia mchezaji huyo kwamba uamuzi huo unatoka katika
wizara ya afya nchini humo.
''kilabu
hiyo imeniambia kwamba sifai kuwa na timu hiyo kwa muda wa siku 15 hadi 21 kwa
kuwa nilienda barani Afrika kucheza na kwa sababu ya virusi vya ugonjwa wa
Ebola'',Kamara aliiambia BBC.
''Wameniambia
wazi kwamba ninafaa kukaa nyumbani ama naweza kusafiri kwenda ughaibuni kuiona
familia yangu lakini si kufanya mazoezi na kilabu hiyo''.
Sierra
Leone ililazimika kuandaa mechi yake dhidi ya Cameroon mjini Younde kwa kuwa
imepigwa marufuku kuchezea nyumbani na shirikisho la soka barani Afrika kutokana
na mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola nchini humo.
(BBC)
Post a Comment