Na EmanuelMadafa,Mbeya
ALIYEKUWA
Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Antony Mwakasungura
amedaiwa kuvunja ofisi ya chama hicho Wilayani humo kwa lengo la kile
kilichodaiwa kutaka kuiba nyaraka mbalimbali za chama.
Tukio
hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii katika ofisi za chama hicho ambapo
inaelezwa kuwa alivunja mlango na kuingia ndani na kudai kuwa alikuwa akichukua
nyaraka zake binafsi.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho Award Kalonga amesema
kuwa Katibu huyo alikuwa akikataa kukabidhi ofisi kwa uongozi mpya
pamoja na kuitwa kwenye vikao vitatu mfululizo kwa ajili ya kufanya
makabidhiano na uongozi mpya.
Amefafanua
kuwa mara baada ya kuingia ndani alianza kupekua baadhi ya mafaili ya ofisi na
mengine kuyachana hali ambayo ilizusha tafrani kiasi cha kusababisha vurugu.
Amesema
kuwa wakati wa tafrani hiyo kiongozi huyo wa zamani alikuwa akitoa maneno ya
kejeli na kutamba kuwa hawawezi kumfanya chochote.
Hata
hivyo mara baada ya kutokea vurumai hiyo kiongozi huyo alifanikiwa kuwakimbia
viongozi hao na kutokomea kusikojuliana.
Kwa
upande wake Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amekiri kuwepo kwa
tukio hilo na kusema kuwa jalada la kesi hiyo linashughulikiwa kwa ajili ya
kufikishwa kwa mwanasheria ili kufikishwa mahakamani.
Post a Comment