Mganga Mkuu wa jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro. |
Na Mwandishi wetu,
ZOEZI la utoaji chanjo ya Surua Rubella, minyoo na
kichocho kwa watoto na watu wazima, Mkoani Mbeya, huenda lisifikie
malengo yake kutokana na shule binafsi za Msingi na Sekondari, kudaiwa kutoa
ushirikiano hafifu kwa serikali kwa kile kinachodaiwa kuhofia wazazi kuwaondoa
watoto wao.
Akizungumzia hilo, Mganga Mkuu wa halmashauri ya Jijiji la Mbeya,
Samweli Lazaro, alisema huenda zoezi hilo lisifanikiwe kwa aslimia 100 kutokana
na ugumu uliopo wakati wa utoaji huduma hiyo kwa watoto walio
shuleni hususani katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Amesema, lengo la serikali kwa Jiji la Mbeya, nikufikia watoto na
watu wazima 630324 ambao watapatiwa chanjo ya Surua Rubella, dawa za
minyo, matone ya vitamini A na dawa zinazokinga Usubi, minyoo ya Tumbo, Matende
na Mabusha kwa kuzingatia makundi yao.
Amesema, ugumu unakuja kwa kundi la watoto walio katika umri wa
miaka 5 hadi 18 ambao asilimia kubwa ni wanafunzi na hasa wanaopata
elimu katika shule za binafsi.
Amesema, hali hiyo inatokana na kasumbua walioyokuwa
nayo baadhi ya wazazi baada ya tukio la Morogoro kutokea la watoto 363 kupoteza
fahamu mwaka 2008 baada ya kupewa dawa ya minyoo na kichocho.
Amesema, hivyo kasumbua hiyo bado imewakaa baadhi ya wazazi jambo
linalowapa ugumu walimu wa shule hizo za binafsi kuruhusu watoto kupatiwa
huduma hiyo kwa kigezo kwamba ni lazima wazazi watoe kibali jambo ambalo ni
changamoto kubwa kwa serikali kutimiza malengo yake.
“Utafiti unaonyesha kwamba walimu au wamiliki wa shule wamekuwa
wakitoa ushirikiano hafifu kwa serikali katika zoezi hili la utoaji wa chanjo
na dawa mbalimbali kwa wanafunzi walio shuleni kwa kuhofia wazazi
kuwaondoa watoto wao hivyo kuathirika kiuchumi,”alisema.
Amesema, shule binafsi zimekuwa zikijiendesha kupitia ada
zinazotolewa na wazazi hivyo shule ikikumbwa na skendo hiyo basi hupoteza sifa
hivyo kusababisha jamii kutoandikisha wanafunzi katika shule hiyo.
Aidha, Dkt. Lazaro aliwaomba walimu pamoja na wazazi
kuondokana na mtazamo huo kwani kinachotakiwa kufanyika ni kutoa elimu kwa
jamii ili kutambua umuhimu wa chanjo na dawa hizo katika mwili wa mwanadamu.
Watoto 171,862 walio katika umri wa miezi 9 mpaka chini ya miaka
15 wanatarajia kupata chanzo ya Surua Rubella, 62772 wenye umri wa miezi 6
mpaka miezi 59 wanatarajia kupewa matone ya vitamin A, dawa za minyoo watoto miezi
12 hadi 59 huku watoto kati ya miaka 5 na kuendelea 345,110 watapatiwa dawa
zinazokinga Usubi, Minyoo ya Tumbo, matende na mabusha.
Mwisho.
Post a Comment