Na
EmanuelMadafa,Mbeya
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya, imetoa kibali cha kukamatwa na kuuzwa kwa
magari matatu ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na Kampuni ya
mawasiliano Vodacom Tanzania, ili kulipa fidia ya shilingi milioni 86,553,700
kwa kosa la kumsababishia mteja hasara baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti
kwa kutumia huduma ya kibenki ya njia ya simu bila idhini
yake.
Kesi
hiyo namba 4 imefunguliwa mahakamani hapo, Mei 13 mwaka huu na mlalamikaji
Mwanswa Jonas dhidi ya Taasisi ya kibenki ya NMB na kampuni ya Vodacom Tanzania
na mahakama hiyo kutoa hukumu Oktoba 13
mwaka huu kwa kutoa kibali cha kuuzwa kwa magari hayo.
Akisoma
shitaka hilo, hivi karibuni, Kalani wa mahakama ya Wilaya ya Chunya Izza
Sheumu, mbele ya hakimu wa Wilaya, Desdery Magezi, alisema, Mei 13,2014 ,
mlalamikaji alibaini kupotea kwa fedha zake zikiwa na thamani ya shilingi
milioni 6,553,700 zilizokuwa kwenye akaunti namba 6071600335 kupitia benki ya
NMB.
Amesema,
uchunguzi ulibaini kuwa fedha hizo zilipotea baada ya kuhamishwa kwa kutumia
huduma ya kibenki ya njia ya simu kutoka akaunti namba 6071600335 kwenda kwenye
namba ya simu ya mkononi ya Vodocom 0768 713668 bila ya idhini ya
mteja.
Amesema,
imeelezwa kuwa wakati zoezi hilo linafanyika mteja huyo alisitishiwa huduma ya
mawasiliano kwa muda na kwamba alipofuatilia kwenye ofisi za Vodacom, alielezwa
kwamba asubiri huduma yake itarudishwa kwani kunamatatizo ya kiufundi.
Amesema,
mlalamikaji huyo akiwa katika harakati za kuweka kiasi cha fedha cha
shilingi milioni 16 kupitia kwenye akaunti yake iliyopo katika benki ya NMB
kabla ya kuweka fedha hizo aliomba salio na kuambia salio lake halitoshi licha
ya akaunti yake kudaiwa kuwa na kiasi cha fedha zaidi ya shilingi
milioni sita.
Amesema,
alipofuatilia alishangazwa kuelezwa kwamba fedha hizo alizitoa yeye kupitia
namba yake ya simu ya mkononi ya Vodocom jambo ambalo alilipinga hivyo kuamua
kupeleka malalamiko yake kwenye ofisi za wanasheria Tanganyika Law Society na
kesi hiyo kusimamiwa na wakili wa kujitegemea, Radlsaus Lwekaza, ambaye
aliiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo, Julai 24, mwaka huu.
Pia,
imeelezwa kuwa wakili, Rwekeza, aliiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo upande
mmoja, kwa kuelezea kwamba wadaiwa wameamua kwa makusudi kutohudhuria na
kujitetea kwenye kesi husika baada ya mahakama kuhairisha kesi hiyo mara nyingi
bila ya wao kutokea licha ya kupelekewa hati ya kuitwa.
Amesema,
baada ya hapo kesi ilisikilizwa upande mmoja, na mahakama hiyo kutoa
hukumu 15/8/2014 ya kwamba mshitakiwa namba moja ambaye ni NMB alipe shilingi
milioni 43, 272,750 na Vodacom alipe milioni 43,272,750 ambapo mdai aliomba
kukazia hukumu baada ya siku 30 za rufaa kupita na mahakama ilimkubalia na
hatimaye Oktoba 13 mwaka huu mahakama ilitoa kibali kwamba magari mali ya NMB
na Vodacom kuuzwa.
Mahakama
hiyo, iliyataja magari hayo kuwa ni gari namba T519 CHP Nissan Patrol nyeupe ,
T947 CVE Toyota Land Cruiser mali ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na gari namba
T388 CGW Nissan Hard Bord mali ya kampuni ya Vodocom.
Aidha,
mahakama hiyo ilitoa kibali kwa Kampuni ya Jagro Enterprices limited,
inayomilikiwa na Maulid Hamis kukamata magari hayo.
Mwisho.
Post a Comment