Mkurugenzi wa Kampuni ya Jagro Enterprice Bw.Maulid Hamis wa kwanza kushoto akijibishana na askari nje ya Benki ya Nmb Mbalizi katika harakati za kukamata gari la benki hiyo . |
Gari la Benki ya Nmb linalotumiwa na benki hiyo ambalo limekamatwa na Madalali hao wa mahakama |
Kikosi kazi cha Jagro kikitekelza majukumu |
Meneja wa Benki ya Nmb Tawi la Mbalizi Mbeya akikatiza mitaa mara baada ya gari lake kukamatwa na madalali wa mahakama. |
Na EmanuelMadafa
Kampuni ya ukamataji wa magari ya ya Jagro Enterprises Limited ya
jijini mbeya imefanikiwa kukamata gari la Taasisi ya Kibenki ya NMB Mbalizi Mbeya.
Ukamataji wa gari hiyo ni utekelezaji wa amri ya Mahakama ya
Wilaya ya Chunya ambayo iliamuru
kukamatwa kwa magari matatu
ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na Kampuni ya mawasiliano Vodacom
Tanzania, ili kulipa fidia ya shilingi milioni 86,553,700 kwa kosa la
kumsababishia mteja hasara baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti kwa kutumia
huduma ya kibenki ya njia ya simu bila idhini yake.
Kesi hiyo namba 4 imefunguliwa mahakamani hapo, Mei 13 mwaka huu
na mlalamikaji Mwanswa Jonas dhidi ya Taasisi ya kibenki ya NMB na kampuni ya
Vodacom Tanzaniana, na mahakama hiyo kutoa hukumu Oktoba 13 mwaka huu kwa kutoa
kibali cha kuuzwa kwa magari hayo.
Akisoma shitaka hilo, hivi karibuni, Kalani wa mahakama ya Wilaya
ya Chunya Izza Sheumu, mbele ya hakimu wa Wilaya, Desdery Magezi, alisema, Mei
13,2014 , mlalamikaji alibaini kupotea kwa fedha zake zikiwa na thamani ya
shilingi milioni 6,553,700 zilizokuwa kwenye akaunti namba 6071600335 kupitia
benki ya NMB.
Alisema, uchunguzi ulibaini kuwa fedha hizo zilipotea baada ya
kuhamishwa kwa kutumia huduma ya kibenki ya njia ya simu kutoka akaunti namba
6071600335 kwenda kwenye namba ya simu ya mkononi ya Vodocom 0768
713668 bila ya idhini ya mteja.
Alisema, imeelezwa kuwa wakati zoezi hilo linafanyika mteja huyo
alisitishiwa huduma ya mawasiliano kwa muda na kwamba alipofuatilia kwenye
ofisi za Vodacom, alielezwa kwamba asubiri huduma yake itarudishwa kwani kunamatatizo
ya kiufundi.
Alisema, mlalamikaji huyo akiwa katika harakati za
kuweka kiasi cha fedha cha shilingi milioni 16 kupitia kwenye akaunti yake
iliyopo katika benki ya NMB kabla ya kuweka fedha hizo aliomba salio na kuambia
salio lake halitoshi licha ya akaunti yake kudaiwa kuwa na kiasi cha fedha zaidi
ya shilingi milioni sita.
Alisema, alipofuatilia alishangazwa kuelezwa kwamba fedha hizo
alizitoa yeye kupitia namba yake ya simu ya mkononi ya Vodocom jambo ambalo
alilipinga hivyo kuamua kupeleka malalamiko yake kwenye ofisi za wanasheria
Tanganyika Law Society na kesi hiyo kusimamiwa na wakili wa kujitegemea,
Radlsaus Lwekaza, ambaye aliiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo, Julai 24,
mwaka huu.
Pia, imeelezwa kuwa wakili, Rwekeza, aliiomba mahakama kusikiliza
kesi hiyo upande mmoja, kwa kuelezea kwamba wadaiwa wameamua kwa makusudi
kutohudhuria na kujitetea kwenye kesi husika baada ya mahakama kuhairisha kesi
hiyo mara nyingi bila ya wao kutokea licha ya kupelekewa hati ya kuitwa.
Alisema, baada ya hapo kesi ilisikilizwa upande mmoja, na
mahakama hiyo kutoa hukumu 15/8/2014 ya kwamba mshitakiwa namba moja ambaye ni
NMB alipe shilingi milioni 43, 272,750 na Vodacom alipe milioni 43,272,750
ambapo mdai aliomba kukazia hukumu baada ya siku 30 za rufaa kupita na mahakama
ilimkubalia na hatimaye Oktoba 13 mwaka huu mahakama ilitoa kibali kwamba
magari mali ya NMB na Vodacom kuuzwa.
Mahakama hiyo, iliyataja magari hayo kuwa ni gari namba T519 CHP
Nissan Patrol nyeupe , T947 CVE Toyota Land Cruiser mali ya Taasisi ya Kibenki
ya NMB na gari namba T388 CGW Nissan Hard Bord mali ya kampuni ya Vodocom.
Aidha, mahakama hiyo ilitoa kibali kwa Kampuni ya Jagro
Enterprices limited, inayomilikiwa na Maulid Hamis kukamata magari hayo.
Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kukamatwa kwa magari hayo,
Mwanasheria wa Kampuni hiyo ya Jagro Bw.Aloyce Mrema amesema kuwa
wanachokifanya sasa ni kutekelza amri ya mahakama ya kukamata magari hayo nakwamba
mchakato wa kuyakamata magari ya Taasisi ya Kibenki ya NMB unaendelea licha ya
akwamba wameamata gari moja.
Mwisho.
Post a Comment