(Picha Maktaba) |
Na Mwandishi wetu ,Mbeya
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu watano kwakosa la kujihusisha na biashara ya na
pombe kali zilizopigwa marufu .
Matukio
ya kukamatwa kwa watu hao yamehusisha maeneo tofauti mkoani hapa ambapo katika
tukio la kwanza, Mkazi wa Mkwajuni Wilaya
ya Chunya Ndugu Prisca Sinkala (31)
alikamatwa akiwa na pombe ya moshi
[gongo] yenye ujazo wa lita 05.
Mtuhumiwa alikamatwa Octoba 22 mwaka huu majira ya saa
12 jioni huko katika kijiji cha mkwajuni, chunya, mkoa wa Mbeya ambapo Mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo
Katika tukio la pili, Mkazi wa Soweto Mbeya Isaya Daron
(27) amekamatwa akiwa na pombe kali [viroba] zilizopigwa marufuku aina ya boss paketi 30 ambapo Mtuhumiwa
alikamatwa Octoba22 mwaka huu majira ya saa
8 mchana huko soweto.
Katika tukio
la tatu,
Mkazi wa airport jijini mbeya aitwaye Ndugu Salehe Sekile (32) anashikiliwa na jeshi hilo akiwa na kete
12 za bhangi sawa na uzito wa gramu
60 ambapo Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo octoba
22 mwaka huu.
Mtuhumiwa alikutwa na kete hizo baada ya
kupekuliwa kwenye mifuko yake ya suruali ambapo mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi hiyo.
Aidha jeshi hilo la polisi mkoa wa mbeya linawashikilia
watu wawili wakazi wa manga jijini mbeya ambao ni Teresia Mwaisakile (31) na Elizabeth londele (29) wakiwa na pombe
ya moshi [gongo] ujazo wa lita 01.
Watuhumiwa kwa pamoja
walikamatwa katika msako uliendeshwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya ambapo
taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao zinaendelea.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi wa polisi Barakael Masaki
anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya/pombe ya moshi pamoja na
pombe kali zilizopigwa marufuku nchini kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari
kwa afya ya mtumiaji.
mwisho
Mwisho.
Post a Comment