Na Mwandishi
wetu.
MCHEZO wa
ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Tanzania Prisons na Simba uliochezwa jana
katika uwanja wa Sokoine Jijini hapa, uligubikwa na vituko kadhaa
vilivyoambatana na hisia za kishirikina.
Hali hiyo
ilitokea pale Simba walipoamua kuvunja utaratibu wa kuingia katika vyumba vya
kubadilishia, kufuatia kukataa kupitia njia yao na badala yao kupita walikopita
timu ya Tanzania Prisons.
Wachezaji wa
Simba walifikia maamuzi hayo baada ya kupokea amri kutoka kwa mtu mmoja
aliyewapa maelekezo baada ya kukaribia eneo hilo la vyumba vya kubadilisha
vilivyopo chini ya jukwaa Kuu ndani ya Uwanja wa Sokoine.
Mtu huyo
ambaye hata hivyo hakuweza kujulikan a mara moja kama alikuwa ni kiongozi wa
timu hiyo, kabla timu hiyo haijafika ndani ya uwanja alionekana kusimama katika
eneo hilo na alipoona wachezaji wa Simba wanaingia uwanjani alijitayarisha na
kuzuia njia ya kuingilia Simba.
Mtu huyo
ambaye muda wote alionekana kusimama kwa ukakamavu wa hali ya juu baada ya
kuona wachezaji wa Simba wamekaribia eneo hilo lakuingilia katika vyumba vya
kubadilishia nguo alionekana kuwatolea ishala wachezaji akiwaelekeza kupitia
upande wa pili huku yeye akiziba njia.
Kutokana na
hali hiyo wachezaji hao wa Simba walitii amri hiyo na kuamua kupitia njia
walioitumia Tanzania Prisons kuingilia katika vyumba hivyo vya kubadilishia na
kasha mwenye kuondoka na kutokomea kwenye jukwaa Kuu.
Katika hatua
nyingine , wachezaji wa Simba katika mchezo huo wakitumia lango Kuu la uwanja
wa Sokoine waliingia wakiwa chini ya ulinzi mkali wa watu wanaodhani kuwa ni
makomandoo wakiyasindikiza magari mawili.
Hata hivyo,
Simba waliingia uwanjani hapo wakiwa kwenye gari aina ya Coaster , huku gari ambalo hulitumia
siku zote likiwa mbele na watu wacheche ambao walionekana ni mashabiki.
Simba tangu
wafike Jijini hapa kujiwinda na mchezo huo walionekana kuwa makini sana na suala la hujuma, ambapo inadai
waliamua kukodi Hoteli yote wakihofia hujuma za aina yeyote.
Mwisho.
Post a Comment