WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, asiye na Wizara
Maalum, Profesa MarkMwandosya akizungumza na waandishi wa habari jijini mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum, Profesa MarkMwandosya,ameshangazwa
na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia fedha katika kutafuta nafasi
mbalimbali za uongozi na kuhoji ya kwamba fedha hizo wanazitoa wapi na kwa
maslahi ya nani.
Amesema
yeye ni maskini hana fedha za kuwanunua wajumbe wa kumpigia kura ifikapo mwaka
2015 lakini ameweka bayana kwamba yupo tayari kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
mkubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la CCM
Mkoa wa Mbeya, kilichokuwa kikipitia na kujadili masuala mbalimbali ya chama
kilichofanyika katika ofisi za CCM zilizopo Jijini humo.
Amesema,
hivi sasa kumeibuka mtindo na imani kwamba fedha ndio msingi wa
uteuzi na kuchaguliwa kwa mtu kuwa kiongozi, jambo linalomtatanisha sana na
kwamba ni kinyume cha misingi na matarajio ya wananchi na ya vyama vya siasa.
Amesema,
wananchi wanafahamu mshahara wake, tangu alipoteuliwa kuwa Waziri hadi
sasa na wanaweza wakaongeza na zile za safari zake zote alizosafiri lakini
hana jeuri ya kuwalipa wajumbe ili wampigie kura.
Amesema,
endapo nafsi yake itamsukuma kuwatumikia wananchi basi itakuwa ni kwa upendo
wake lakini si kwasababu ya kwamba yeye anafedha na
angependa kutangaza kwamba fedha hizo hana ila yeye matumaini yake
makubwa ni hali aliyokuwa ambayo inatokana na kuafanana na wananchi.
Amesema,
ni vema wahusika hao wakazielekeza fedha hizo kwa wananchi kwa kuwapatia
thamani halisi kupitia kwenye hospitali na vituo vya afya kwa matumizi ya dawa
na kununua mabati dawa , vituo vya afya kuwekewa mabati kuliko kushusha thamani
ya mtu na kumfanya mtumwa kupitia fedha zako.
Amesema,
wakati umefika kwa jamii kurudi kwenye siasa za kizamani kuliko
kumrubuni mwananchi kwa uongozi kupatikana kwa njia ya fedha, fedha ambazo
hujui zimetoka wapi na zitarudishwa kwa njia ipi.
Amesema,
siasa ya sasa imekuwa ni ya watu wenye fedha au watu waliogeuzwa
mawakala kutokana na fedha za watu fulani bdala ya siasa ya wafanyakazi na
wakulima ambayo ndiyo iliyokuwa ikipiganiwa na Mwalimu pamoja
Karume.
Hata hivyo amesema nivema kutambua kuwa hatua ya kumchagua mtu kuwa rais kupitia chama cha Mapinduzi ni hatua ngumu sana kwani huyo ndiyo anayetegemewa kuwa mwenyekiti wa chama hicho hivyo si suala la kukurupuka tu.
Mwisho.
Post a Comment