Na Mwandishi wetu,mbeya
TIMU ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro, imejiimarisha kileleni mwa ligi Kuu ya Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa bao 2 -0 dhi ya Mbeya City, katika uwanja wa Sokoine Jijini hapa.
Pambano hilo ambalo kila timu ililichukulia kwa umuhimu wake, wakati Mtibwa wao wakita kupanda ushindi ili kuendelea kujiimariosha kileleni, huku Mbeya City wao wakitaka kurudisha hadhi yao.
Hata hivyo, Mtibwa ndio walijikuta wakinufaika na mchezo huo baada ya mshambuliaji wake, Amme Abdalah, kuifungia bao la kwanza katika dakika ya 21 baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na David Luhende.
Lakini Mtibwa nao waliendelea kusukuma mashambulizi kwa wapinzani wao wakiongozwa na kiungo wao wa pembeni Mussa Hassani Mgosi, hivyo hadi Mapumziko, mtibwa walifanikiwa kuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kilianza kwa mikimiki ya mashambulizi, hali iliyosababisha mabeki wa Mtibu kuwa kwenye wakati mgumu na beki wake wa kushoto David Luhende kupewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Deus Kaseke.
Katika hali ya kutaka kujiimarisha zaidi ili waweze kurudisha bao hilo, dakika ya 58 Kocha Mkuu wa Prisons, Juma Mwambusi, alimtoa Saad Kipanga na kumuingiza, Peter Mapunda, lakini ma,mbo hayakubadilika na Mtibwa waliendelea kuwashambulia.
Mtibwa nao katika dakika ya 68 walimtoa Mussa Mgosi na kumuingiza Vicent Salamba, ambaye dakika kumi baadae aliipatia Mtibwa bao la pili, liliwamaliza nguvu wachezaji wa Mbeya City .
Hivyo hadi mwamuzi wa mchezo huo, Hashimu Abdalah, kutoka Dar es salaam anamaliza mchezo huo, Mtibwa waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Katika hali nyingine , mara tu baada ya bao hilo kufungwa mashabiki wa Mbeya City walianza kutoka uwan jan I huku wakirusha chupa za maji kwa kile kilichoonekana hasira za timu yao kutofanya vizuri msimu huu.
Mtibwa imejiimarisha zaidi kileleni mwa ;ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 13, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10 baada ya juzi kufungwa bao 1-0 na JKT –Ruvu nyumbani kwake Chamanzi.
Kiungo Msambuliaji wa Mbeya City Paul Nonga akilia kwa uchungu mara baada ya timu yake kufungwa na Mtibwa katika uwanja wa sokoine jijini mbeya |
Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakimfariji kipa wa Mbeya City Davd Buruhan |
Mashabiki na wachezaji wa Mbeya City wakitoka nje ya uwanja kuelekea kambini kwa miguu. |
Post a Comment