Na Mwandishi wetu,
Mtoto umri wa mwaka mmoja na nusu [011/2] aliyetambulika
Ndugu Elisha Juma mkazi wa shewa amefariki dunia baada ya kutumbukia
kwenye kisima chenye maji machafu.
Tukio hilo limetokea Octob 23 mwaka huu majira ya saa 07:00 asubuhi katika Mtaa shewa, kata ya mwakibete jiji mbeya.
Inadaiwa kuwa, kabla
ya tukio hilo, marehemu alikuwa akicheza maeneo ya jirani na kisima hicho
kilichokuwa na maji machafu ya mvua yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa ajili ya
shughuli za ujenzi.
Mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya kwa ajili ya uchunguzi wa
kitabibu.
Kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi Barakael Masaki anatoa wito kwa wazazi walezi kuwa makini na watoto
wadogo ikiwa ni pamoja na kuweka uangalizi wa kutosha ili kuepuka madhara
yanayoweza kuepukika.
Aidha, anatoa wito
kwa jamii kufukia mashimo, kufunika visima na matundu ya maji machafu kwani ni
hatari kwa watoto wadogo.
Mwisho.
Post a Comment