Mtanange unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Mkoa wa Mbeya kati
ya timu za Simba Fc na Tanzania Prisons,
ambao unaotalajiwa kutimua vumbi ndani
ya uwanja wa sokoine 0ctoba 25 mwaka huu mchezo huo umeendelea kuchukua sura mpya katika vitongoji vya jiji la mbeya ambapo
mpaka sasa timu hizo zimegoma kuutumia uwanja huo wa sokoine kwa ajili ya mazoezi kutokana na
sababu zisizoeleweka.
Timu ya Simba, imewasili Jijini Mbeya juzi, kwa kutumia usafiri wa
ndege na kufikia hotel ya Padz , imedaiwa kugoma kuutumia uwanja wa
Sokoine kwa ajili ya mazoezi na kutafuta kiwanja kingine.
“Timu ya Simba Fc, imewasili Mbeya juzi na kufikia
hotel ya Padz na kwamba siku (leo) kwa utaratibu wa TFF inatakiwa kuutumia
uwanja wa Sokoine kwa mazoezi lakini hatuta utumia kutokana na
sababu za kiufundi,”kilisema chanzo hicho cha habari ambacho kiliomba
kutoandikwa jina lake.
Kilisema, mwenendo wa timu hiyo
bado haujakaa vizuri kutokana na kutoa sare nne ndani ya mechi nne
hivyo ni vema ikajiwekea ulinzi wa kutosha katika kutafuta pointi tatu ambazo
ndizo zimewaleta Mbeya.
Aidha, kwa upande wa timu ya Tanzania Prisons, imeelezwa, licha
ya timu hiyo kuwa wenyeji wa uwanja huo lakini nao wameonekana kutoutumia uwanja
huo kufanyia mazoezi kwa maelezo kwamba ndio desturi yao kutokana na kutumia
kiwanja chao kilichopo ndani ya Jeshi la Magereza.
“Sisi hatuna sababu ya kutumia uwanja wa Sokoine kwa mazoezi kwani
tumekuwa na kiwanja chetu ambacho tunakitumia mara kwa mara lakini hii
haituzuii kukilinda kiwanja hiki ,”alisema John Mwakitange mdau wa timu ya
Tanzania Prisons.
Amesema, timu yetu kwa sasa imepoteza mvuto kwa mashabiki wetu
kutokana na kuruhusu kufungwa na Ruvu Shot , hivyo mechi dhidi na Simba ni
lazima tujipange kwa kila njia ili kuhakikisha tunawarudisha
mashabiki wetu pamoja na kutokubali kuvunja rekodi tuliyonayo juu ya Simba hasa
timu ikiwa nyumbani.
Mwisho.
Post a Comment